ACT wafanikiwa kuchukua kiti kingine cha Udiwani Kagera! - LEKULE

Breaking

16 Nov 2015

ACT wafanikiwa kuchukua kiti kingine cha Udiwani Kagera!

1


[TANZANIA] Chama cha ACT upitia mtandao wake wa Twitter wametaarifu kuwa chama hicho kimefanikiwa kutwaa nafasi ya kiti cha Udiwani kupitia Kata ya Kagera, iliyopo katika mji wa Kigoma Ujiji, Mkoani Kigoma.
Kupitia kwenye akaunti yao hiyo ya chama hicho ya ACTwazalendo (Taifa kwanza) wameandika:
#Uchaguzi uliofanyika Leo kata ya Kagera ACTwazalendo tumeshinda kwa kishindo kikubwa tunawashukuru sana kwa kutuamini na kutupatia Diwani.” ulisomeka ujumbe huo.
Chama hicho kwa sasa ni miongoni mwa vyama vikuu vya upinzani nchini hasa kwa harakati zake za kisiasa kwa kujizolea wanachama mbalimbali karibu Tanzania nzima huku kikiongozwa na Mwanasiasa machachari, Mh. Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni Mbunge mteule wa kupitia jimbo la Kigoma Mjini.
Hadi sasa ACT wamefanikiwa kuunda Halmashauri ya Kigoma Ujiji.

No comments: