ALIYEKUWA
mgombea ubunge Jimbo la Ilemela, Highnes Kiwia, kwa tiketi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametangaza kwenda mahakamani kupinga
matokeo yaliompa ushindi, Angelina Mabula (CCM).
Kiwia
amesema kuwa matokeo yaliyompa ushindi Mabula yalikuwa ni ya
kutengenezwa ili kumbeba mgombea huyo wa CCM kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kiwia amesema atatumia haki ya kikatiba
kupinga matokeo hayo mahakamani ili maoni ya wananchi kuheshimiwa na
kupata haki zao za msingi.
Hata
hivyo katika matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, John Wanga,
alimtangaza Angelina Mabula mshindi kwa kura 81, 424 dhidi ya Kiwia
aliyepata kura 61,679.
Kiwia
pia amesema kuwa katika baadhi ya vituo majina ya wapiga kura
yaliongezwa, mawakala wake kutishiwa na baadhi ya wafuasi wa CCM kitendo
ambacho dhahili alidai uchaguzi haukuwa huru.
“Kuna
vituo ambavyo majina yaliongezwa, zaidi ya majina 700 ya wapiga kura
yalihamishwa na kupelekwa Ukerewe, baada ya kupata taarifa ya kuhamishwa
majina tulitoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi lakini hatua
hazikuchukuliwa.
“Matokeo
haya yalikuwa yamepangwa kabla ya uchaguzi kufanyika, tunaenda mahakani
kupinga matokeo haya, hatutaona maoni ya wananchi yanapotea,” amesema Kiwia.
Pia
Kiwia alivitaja baadhi ya vituo ambavyo vilikuwa na kasoro kuwa ni
pamoja na Kitangiri, Ilemela na Nyansaka na kwamba wamejipanga muda
wowote kwenda mahakamani.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Chadema, Kanda ya Ziwa Victoria, Tungaraza
Njugu amesema matokeo ya uchaguzi huo sio sahihi na kwamba maoni ya
wananchi walio wengi yameporwa na CCM.
No comments:
Post a Comment