Katika mitandao ya kijamii leo taarifa ilisambaa kuwa Jongo Salum maarufu kama Dr. Manyaunyau amefunguliwa mashtaka ya utapeli na kutakiwa kwenda jela miaka mitatu sambamba na fidia ya zaidi ya milioni 2.
Mwenyewe leo kaweka wazi ukweli wa mambo na kusema habari hizo si za kweli kwa kuwa kuna mtu ambaye anatumia jina lake na kuwadanganya watu.
Kazi alizowahi kufanya Dr. Manyaunyau kabla ya kufanya kazi ya uganga...
”Nimepitia katika changamoto nyingi, kwa ufupi kabla ya kuanza kazi hii aliwahi kuwa mpiga debe, kuvua samaki, msanii wa kundi la Kaole na nilifanya kazi na kina Dr. Cheni na Swebe, na sikuwahi kufikiria sana kama ningekuwa mganga lakini wazee wangu ndio walikuwa wakinisumbua wanirithishe kazi zao”….Dr. Manyaunyau
“Wazazi wangu waliniacha nikiwa mdogo na nilikutana na changamoto nyingi katika kuyakabili maisha, nimelala nje baada ya ndugu zangu kunifukuza na wakati mwingine nilikuwa nauza simu mbovu na matokeo yake naishia polisi” aliongeza.
Kuhusu familia Dr. Manyaunyau amesema ..
“Familia ninayo, nimejaliwa kuwa na watoto wawili lakini mpaka sasa sijaoa”
Jinsi jina lake linavyotumiwa na matapeli..
“Hili tukio la jana kudaiwa nimeshtakiwa si kweli na mimi sina kesi wala hakuna mtu anayenidai, nafuata taratibu zote na nina vibali vyote vinavyotakiwa, wapo watu ambao wamekuwa wakitumia jina langu vibaya ili kujipatia umaarufu, mimi nasema nafanya kazi zangu vizuri kusaidia jamii na si kingine”.
“Kuna mtu alifanya shughuli zake za uganga na kutumia jina langu, baada ya kushindwa kufanya kile alichotakiwa alishtakiwa lakini si mimi, naomba Watanzania waelewe hili, wapo wengi hata wengine wapo Mikoani ambao wamekuwa wakitumia jina langu, nimekuwa nikijiuliza wanatumia kwa sababu ipi lakini sijapata jibu.. labda lina mafanikio kwao”…
Kuhusishwa na masuala ya ushirikina na wasanii wa muziki..
“Unajua wengi wanatuweka katika kundi la washirikina sio kweli, sisi tunaomba kwa njia aina mbili, za jadi na vitabu, watu wanapokuja wanataka kuombewa, pia wasanii wengi wamekuwa wakija kwa ajili ya kuombewa dua kwa mfano anapotaka kutoa album au nyimbo yake ifanye vizuri.. hilo kwangu ni la kawaida”..Dr. Manyaunyau
Anazungumziaje uongozi mpya wa Serikali ya Awamu ya tano?…
”Kwa sasa nimeona kuna mabadiliko, lakini ndio mwanzo siwezi kutolea maamuzi kabisa, labda tusubiri baraza la Mawaziri na nini watafanya katika kutufikisha mahali ambapo Watanzania wanataka kufika”..
Hapa kuna SAUTI ya Dr. MANYAUNYAU wakati wa mahojiano..
No comments:
Post a Comment