Wabunge wapya kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wanaotarajia kuingia Bungeni wiki ijayo wametakiwa kupigania kupatikana kwa katiba mpya itakayowezesha kupatikana kwa tume huru ya taifa ya uchaguzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya Shinyanga mjini Bw. Samson Ng’wagi amesema kwamba wabunge wa ukawa waliopata nafasi ya ubunge wanatakiwa kusimamia upatikanaji wa katiba mpya ambayo itasaidia kuwa na tume huru ya uchaguzi ili kuondoa hali ya sintofahamu katika chaguzi zijazo kutokana na tathimini ya uchaguzi uliopita.
Ameongeza kuwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa vijana hawakuridhishwa na mwenendo mzima wa uchaguzi kwa madai ya kuwepo hujuma na vitendo vya rushwa kutawala pamoja na vyombo vya dola kutumika kukisaidia chama tawala ili kiendelee kubaki madarakani..
Kwa upande wake Katibu wa BAVICHA wilaya ya Shinyanga mjini Zainab Heri ameitaka Tume ya uchaguzi Zanzibar(ZEC) imtangaze Maalim Seif kuwa ndiye mshindi wa Urais aliyechaguliwa na wananchi kuliko kufanya vitendo vinavyoashiria kubaka demokrasia.
No comments:
Post a Comment