15 Nov 2015

Aangukiwa na kifusi na kufariki, Chakechake Pemba

 WANANCHI mbali mbali wa mji wa Chake Chake wakiangalia fusi lililomfunika marehemu Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi, baada ya kufunikwa na fusi la mawe baada ya kuporomoka wakati walipokuwa wakichimba msingi wa nyumba ya Ghorofa katika soko la Katari Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 FUSI la mawe lililoporomoka na kusababisha kifo cha kijana Seif Kibishi (33)mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, katika eneo la soko la katari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 ASKARI wa kikosi cha zimamoto na uwokozi Chake Chake Pemba, wakivunja mawe kwa kutumia nyundo, ili kufukuwa fusi lililomfunika kijana Seif Kibishi(33)na kupelekea kupoteza maisha, baada ya fusi hilo la mawe wa fondesheni ya jingo la ghorofa, kumwangukia wakati alipokuwa akichimba msingi yeye na wenzake wanne katika soko katari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 ASKARI wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba wakiweka ulinzi katika eneo lililoporomoka fusi la mawe na kusababisha kifo cha kijana Seif Kibishi (33)mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, huku vikosi vya uokozi vilipokuwa vikifanya kazi ya kufukuwa fusi hilo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla mwenye baibui, akiangalia kazi ya ufukuaji wa mwili wa kijana Seif Kibishi (33) mkaazi wa kibirinzi Chake Chake, iliyokuwa ikifanywa na vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama mkoa huo huko katika soko la katari.

No comments:

Post a Comment