WANANCHI mbali mbali wa mji wa Chake Chake
wakiangalia fusi lililomfunika marehemu Seif Kibishi (33) mkazi wa Tibirinzi,
baada ya kufunikwa na fusi la mawe baada ya kuporomoka wakati walipokuwa
wakichimba msingi wa nyumba ya Ghorofa katika soko la Katari Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
FUSI la mawe lililoporomoka na kusababisha kifo cha
kijana Seif Kibishi (33)mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, katika eneo la soko la
katari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
ASKARI wa kikosi cha zimamoto na uwokozi Chake Chake
Pemba, wakivunja mawe kwa kutumia nyundo, ili kufukuwa fusi lililomfunika
kijana Seif Kibishi(33)na kupelekea kupoteza maisha, baada ya fusi hilo la mawe
wa fondesheni ya jingo la ghorofa, kumwangukia wakati alipokuwa akichimba
msingi yeye na wenzake wanne katika soko katari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
ASKARI wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba wakiweka
ulinzi katika eneo lililoporomoka fusi la mawe na kusababisha kifo cha kijana
Seif Kibishi (33)mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake, huku vikosi vya uokozi
vilipokuwa vikifanya kazi ya kufukuwa fusi hilo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid
Abdalla mwenye baibui, akiangalia kazi ya ufukuaji wa mwili wa kijana Seif
Kibishi (33) mkaazi wa kibirinzi Chake Chake, iliyokuwa ikifanywa na vikosi
mbali mbali vya ulinzi na usalama mkoa huo huko katika soko la katari.
No comments:
Post a Comment