Saa chache baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kumtangaza Ester Bulaya wa Chadema kuwa mshindi katika jimbo la Bunda Mjini, aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo na mpinzani wake mkuu Stephen Wassira amejitokeza na kupinga matokeo hayo.
Wassira amedai kuwa matokeo hayo sio halali na kwamba kuna hujuma zimefanywa ili kumuangusha na kumpendelea Esther Bulaya.
Wassira
ambaye pia alikuwa Waziri wa Chakula na Ushirika, amedai kuwa matokeo
yaliyotangazwa yana kasoro kubwa ikiwa ni pamoja na idadi ya kura
zinazoonekana kuwa zilipigwa zinazidi jumla iliyopo kwenye matokeo hayo.
Alisema
kuwa msimamizi wa uchaguzi alimhujumu kwa kuongeza tarakimu kwenye
matokeo hayo na kwamba tarakimu hizo zilipelekea idadi ya wapiga kura
kwenye kituo kimoja kuzidi idadi iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi. Mwanasiasa huyo mkongwe pia amedai kuwa msimamizi wa uchaguzi
alitangaza matokeo bila kuzingatia sheria ya uchaguzi.
Ester
Bulaya na Wassira ni mahasimu wakubwa wa kisiasa ambao walianza
ushindani mkubwa katika jimbo hilo tangu Ester Bulaya alipokuwa mbunge
wa viti maalum kwa tiketi ya CCM.
No comments:
Post a Comment