Shirika
la utangazaji la Ujererumani,DW limeripoti leo mchana kuwa idadi
kubwa ya watu wameanza kuondoka mkoani Mtwara wakihofia hali ya
usalama wakati wa uchaguzi.
Kwa mujibu wa Dw,watu
wengi wanaoondoka ni wanawake na watoto, hali ambayo inaelezewa
inatokana na vurugu za gesi za mwaka 2013, kuonekana kwa baadhi ya
vifaa vya jeshi na wanajeshi wakiwa kwenye vifaru.
Idadi ya watu wanaondoka katika mkoa wa Mtwara nchini Tanzania wakihofia
hali ya usalama wakati wa uchaguzi imeongezeka na kuzidi kuongeza hofu
katika jamii huku wengi wanaondoka katika mkoa huu ni wanawake na
watoto, hali ambayo inaelezewa inatokana na kutokea kwa vurugu za gesi
mwaka 2013 na kuonekana kwa baadhi ya vifaa vya jeshi na wanajeshi
wakiwa kwenye vifaru.
No comments:
Post a Comment