WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA MAENEO MBALIMBALI YA JIJINI DAR - LEKULE

Breaking

25 Oct 2015

WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA MAENEO MBALIMBALI YA JIJINI DAR

 
Wasimamizi wa uchaguzi wakiendelea kuwahudumia wananchi waliofika katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama leo jijini Dar kwa ajili ya kupiga kura.Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog

Mmoja wa wazee akisaidiwa na mtu wake wa karibu ili kupiga kura katika kituo cha Chuo cha Ustawi wa Jamii  jijini Dar leo
Mlemavu akisaidiwa na mtu wa karibu alipofika katika kituo cha Kenton kwa ajili ya kupiga kura.
Mmoja wa wananchi akiwa kwenye sehemu ya kupigia kura katika kituo cha kupigia kura kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama leo jijini Dar.
Wananchi wakihakiki majina yao katika kituo cha Shule ya Sinza  Mapambano jijini Dar leo.
 Wananchi  wakibadishana mawazo walipokuwa kwenye foleni wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shule ya Sinza  Mapambano jijini Dar leo.
 Wananchi wakihakiki majina yao katika kituo cha Shule Kenton Mwenge jijini Dar leo
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha cha Shule ya Sinza Mapambano jijini Dar leo.
  
 
   Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Sinza  Mapambano jijini Dar leo.
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shule Kenton Mwenge jijini Dar leo
   Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Chuo cha Ustawi wa Jamii  jijini Dar leo

Umati mkubwa ukiwa kwenye foleni katika katika kituo cha kupigia kura kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama leo jijini Dar.
 Rukia Omari (kushoto), akimsaidia kupiga kura jamaa yake Mwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho wakati wa kupiga kura katika kituo cha Mbagala Misheni Dar es Salaam leo asubuhi.
  Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shimbwe Mbagala Kuu.
 Hapa wakihakiki majina yao.
 Mkazi wa Njia ya Ng'ombe Mbagala Kuu, Sarah Simba akipiga kura katika kituo cha Shimbwe Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuwachagua viongozi wake, Rais, Mbiunge na Diwani.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mbagala Kuu.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bwawani Mtoni Kijichi leo asubuhi.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.

 Wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Mbagala Misheni wakiwa kazini.
Msimamizi wa uchaguzi Mkuu katika kituo cha Mbagala Misheni, Yona Komba (kulia), akimpaka winoMwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho baada ya kumaliza kupiga kura katika kituo hicho Dar es Salaam  leo asubuhi. Kushoto ni binti aliyemuomba amsaidie kupiga kura  Rukia Said.

No comments: