Na Mwandishi Wetu, Arusha.
VITU
vinavyofanya wanafunzi kwenda kusoma nje ya nchi ni kutokana kozi
wanayoenda kusoma zina uwigo mkubwa wa ajira ambapo vyuo vya ndani
havina kozi hizo.
Akizungumza
na katika kongamano la saba la vyuo vikuu la kujadili mstakabali wa
elimu nchini, lililofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita,
Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL), Abdulmaliki Mollel amesema
kuwa wanafunzi kwenda nje inatokana na kuangalia fursa za kusoma huko
ambazo nchini hazipatikani nchini.
Amesema
kuwa changamoto nyingine inatokana na masomo waliochagua kutokana na
uchaguzi mdogo kutokana na vyuo inawafanya wanafunzi watafute vyuo vya
nje ili waweze kusoma na kuwa na uhakika wa ajira.
Mollel
amesema katika mazingira ya sasa teknolojia ya kufundisha wanafunzi ni
finyu ukilinaganisha na vyuo vya nje kutokana na uwekezaji katika elimu
ambayo hauwezi kuwa sawa na uwekezaji wa vyuo vya ndani.
Aidha
amesema kuwa ufundishaji wa wanafunzi wa vyuo vya nje unatofautiana
hivyo wazazi kuwa na ushawishi wa kuwekeza elimu kwa watoto wao kutokana
na vyuo vya nje vimewekeza kwa wahadhiri kwa wanafunzi wanne Profesa
mmoja.
Mollel
amesema kuwa kuna kozi zilizopo nchini zinafanya watu wasiweze
kuajirika kutokana na mabadiliko ya elimu zimebaki pale pale bila
kuongezea vitu mbadala ambayo ni tofauti na vyuo vya nje vimweza katika
fani zilizopo nchini hazina ajira wameongeza vitu na kufanya watu watake
kusoma vyuo vya nje
“Maisha
yanabadilika mwanafunzi akisoma ndani na kuona aliyesoma nje ana uwigo
wa ajira inawafanya kuwashauri wazazi wao kwa waliobaki wasome nje ili
waweze kuona mafanikio ya ajira yake” amesema Mollel.
Ameongeza
kuwa kutokana na vyuo kuwa na kozi mbalimbali ambazo kwa sasa haziwezi
kutoa fursa GEL inaweza kuunganisha na vyuo vya nje kuweza kuingiza
mtaala katika vyuo vya ndani kwa kuingia mikataba ambayo itasaidia
vijana wanaohitimu kuwa na uwigo ajira na uwezo wa kujiajiri.
Mollel
amesema GEL imeweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wanaosoma nje kwa
kufanya ufatiliaji juu ya maendeleo yao na wanavyorudi wamekuwa na uwigo
wa kuajirika na kufanya wachague kazi kutokana na maarifa walioyapata
nje.
Mkutano
wa kujadili mstakabali wa elimu nchini uliyoandaliwa na wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana naTume ya Vyuo Vikuu nchini,
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa
vyuo Vikuu nchini (CVCPT) ulionza na Oktoba 1 na kumalizaka oktoba 2
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment