14 Oct 2015

WANAFUNZI NA WALIMU BORA WA MASOMO YA SAYANSI WANEEMEKA NA NMB

1
Meneja Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria (kushoto) akimkabidhi Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawii wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando (kulia) tuzo ya mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kwa niaba ya wanafunzi nane na walimu wanne bora wa masomo ya biolojia na kemia.
2
Meneja Mwandamizi wa Benki Upande wa Taasisi NMB, Noelina Kivaria akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita katika hafla ya utoaji tuzo.
3
Afisa Mauzo wa NMB, Joseph Mang’ongo akimuonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Aya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando kadi ya akaunti ya chapchap wakati wa maonesho yaliyokwepo katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa.(P.T)

4
Wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa katika hafla ya kuwakabidhi tuzo kwa kuibuka vinara iliyofanyika mwishoni mwa wiki  katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
5Picha ya pamoja ya meza kuu, Uongozi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na wanafunzi na walimu katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi na walimu bora wa masomo ya biolojia na kemia kitaifa kidato cha nne na sita jijini Dar es Salaam.

Katika kutambua jitihada za wanafunzi na walimu nchini, Benki ya NMB imewatunukia tuzo wanafunzi nane waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya biolojia na kemia kitaifa na walimu wanne waliowawezesha wanafunzi hao kuwa vinara katika masomo hayo tuzo ya jumla ya shilingi milioni 10  mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kila mwanafunzi aliefanya vizuri zaidi kwenye masomo hayo mawili amejishindia jumla ya shilingi milioni 1 na kila mwalimu shilingi laki 5.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Upande wa Taasisi - Noelina Kivaria alimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Bi.Kivaria aliwapongeza wanafunzi hao kwa jitihada zao shuleni na kuwaasa wanafunzi wengine wachukulie hiyo kuwa ni sehemu ya changamoto kwao hivyo wakaze kamba ili nao waweze kuwa vinara katika masomo yao.
Benki ya NMB imekuwa ikiipa sekta ya elimu nchini kipaumbele cha hali ya juu kwa kushirikiana na shule mbalimbali ndani na nje ya Dar es Salaam ikitoa misaada mbalimbali kama madawati.
Wanafunzi waliotunukiwa tuzo hizo ni:
  1. Samwel Felician-Nyamanoro Secondary School
  2. Jenipher Naali-St. Francis Secondary School
  3. Joshua Zumba-Uwata Secondary School
  4. Monica Mtei-Marian Girls Secondary School
  5. Felister Silvester-Ifunda Tech. School
  6. Mariam Mzingi-Feza Girls Secondary School
  7. Elisha Mmari-St. Mary Goreti Secondary School
  8. Innocent Yusufu-Feza Boys Secondary School
Walimu waliotunukiwa tuzo ni:
  1. Halima Tajiri-Feza Girls Secondary School
  2. Rogasian Fisso-Uwata Secondary School
  3. Grolius Rwabutomize-St. Mary Goreti Secondary School
  4. Jane Lalika-Marian Girls Secondary School

No comments:

Post a Comment