WA AHMADIYYA WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI - LEKULE

Breaking

5 Oct 2015

WA AHMADIYYA WATAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI


Makamu mwenyekiti wa tume ya haki za Binaadamu na utawala Bora Tanzania Iddi Mapachu, alitoa witohuo wakati akiwahutubia waumini wa Dhehebu la Jumuiyya ya Waislam wa Ahmadiyya katika mkutano wa 46,ulioanza tar 2-4 Oktoba katika kijiji cha Kitonga kata ya Msongola wilaya ya Temeke Dar es salaam.
akiongea na wauminihao awali alisema,natoa pongezi za dhati kwa uongozi mzima wajumuiyya na wanajumuiyya kwajumla binafsi nimefurahishwa sana na mualikohuu adhimu napamoja na kupata nafasi yakuhubia,
Hivyo nachukuanafasihii kuitambulishakwenu Tume ambayo ni Idara huru ya serikali iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha 129(1)(c) cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Tume ya haki za binadamu na utawara Bora namba 7 ya Mwaka 2001.
Jukumu kubwa la tume ni kulinda,kutetea na kuhifadhi haki za Binadamu nchini,katika kutika kutekeleza jukumu hilo tme imepewa mamlaka ya kupokea malalamiko,(kwanjia mbalimbali) kutoka kwa mtu yeyeote au kuanzisha uchunguzi wake yenyewe endapo itaona kuna uvunjifu wa haki za binaadamu.
alisema nakama kuna ukiukwaji wa misingi ya utawala bora tume ina wajibu wakutoa elimu kwa umma juu ya uzingatiaji wa haki za binadamu na Misingi ya utawala bora, kifungu cha kwanza cha Tamko la Kimataifa la Haki za binadamu la Mwaka 1948 kinachosema.
"Watu wote wamezaliwa huru,wakiwa na hadhi na haki sawa,wamejaliwa akili dhamiri na kupaswa kutendeana kwaroho ya Kidugu" Haki za msingi ambazo kila mtu anastahili kuwa nazo na kuishi bila kubaguana kwa rangi,taifa,jinsia,dini,siasa,fikra,asili ya taifa la mtu,mali kwa kizazi au kwa hali nyingine yeyote.
akiendelea kufafanua sheria hiyo alisema Kuna tamko lakimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948 linatambua wajibu wa kila mtu na kilajamii katika ulinzi wa haki za binadamu.
ikiwa na malengo makuu mawili moja inadhamiria kuondoa vitendovya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwapa watu mwanga,Pili inalenga kumuwezesha kila mdau kutokana na nafasi yake katika jamiihusika kuweza kujenga uwezo wa kutetea na kukuza haki za binadamu.
Mchango wa viongozi wa Dini. akiendele na na hotuba yake Iddi Mapachu anaeleza Viongozi wadini katika jamii yoyote ile wamekuwa wakipewa nafasi kubwa hasa katika ujenzi wa jamii bora yenye amani,maelewano usawa na maendeleo.
Nawaomba na kusisitiza Viongozi wa dini kuendelea kuimarisha juhudi za kuhubiri Amani,Usalama, maendeleo endelevu na haki za binadamu nchini kote kwani kwakufanyahivyo mtaifanya jamii ishiriki kulinda amani na utulivu ikiwa niwajibu wa kila Mtanzania.
tunatakiwa kutendeana haki,hakindio inayozaa amani kwasababa haki hulinda maisha yetu,Basi sote kwa umojawetu tuwaombee viongozi wetu watende haki,piananinyi viongozi wa dini tutambue wajibu wetu mbele ya Mungu.
Nawakati wowote isipo tendeka ni wajibu wa viongozi kuwa sauti ya wale wasio na sauti,naomba kuanzia sasa Jumuiyya ya Waislamau wa Ahmadiyya ishirikiane na Tume ya Haki za binadamu kuimarisha ushirikiano ili kuona haki inaendelea kwa watu wote.
ALBINO
Akijibu maswali ya waandishi kuhusu matukioya mauaji ya albino hapa nchini, alisema yana dalili ya kupungua kwanimpaka sasa toka juni nitukiomoja tu,ndio limelipotiwa mpakasasa ninaimani elimu inaingia taratibu,
UCHAGUZI
Makamu mwenyekiti wa Tume Iddi Mapachu alisema nawakumbusha wajumbe wa mkutanohuu muhimu,msisahau kuiombea nchi yetu amani katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi mkuu nina ungana na waumini wa dini zote kuiombea amani nchiyetu katika zoezihili, pia tuendelee kuwasihi viongozi wetu wa siasa kuachana na kauli za chuki nazinazo ashiria uvunjifu wa amani tuendelee pia kuwaombea wananchi kuwa watulivu kabla na baada ya uchaguzi,
Kwa upande wake Amir na mbashiri mkuu wa jumuiya ya waislam wa ahmadiyya shekh Tahir Choudhry alimshukuru makamu mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu kuhudhuria mkutano huo na kusema kuwa wa ahmadiyya wanaungana nao ktk kazi wanayoifanya kutokana na ukweli kuwa Mafundisho ya dini ya kiislamu yanasisitiza haki na uadilifu kwa kutambua kuwa huo ndio msingi mkuu wa maendeleo ya kweli kwa mwanadamu hivyo aliwasisitiza waumini wa dini ya kiislamu kuwa mstari wa mbele kutekeleza uadilifi kwa vitendo ili wawe mfano mwema kwa jamii kama alivyofanya Mtume Muhamad S.A,W
Kuhusiana na suala la amani, sheikh Choudhry alisema jumuiya ya waislamu wa ahmadiyya inasisitiza umuhimu wa kustawisha amani kwa jamii kama maana halisi ya jina lenyewe la ISLAM (amani) na kauli mbiu ya Ahmadiyya inavyosema (Upendo kwa wote chuki si kwa yeyote), katika kudhihirisha hilo, jumuiya yao inahubiri amani katika hotuba zake mbalimbali zinazotolewa kote duniani na kiongozi mkuu wa jumuiya hiyo Khalifatul Masih Mirza Masroor Ahmad na hapa Tanzania tayari wameshafanya mikutano ktk mikoa kumi na tano mfano DSM, SHINYANGA, KIGOMA, MOROGORO n.k ikiwahusisha viongozi mbalimbali wa dini na serikali kwa lengo la kuihamasiha jamii kustawisha amani iliyopo kwani panapokuwepo na amani ndio waumini wanapata wasaa wa kutosha kumuabudu mungu na huo ndio msingi mkuu wa dini yetu.
Baada ya hapo makamu mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora akapata fursa ya kukutana na waandish wa habari kujibu hoja kadhaa ikiwemo vitendo vya vyombo vya Dola kuwa na dalili za kunyanyasa wananchi katika mikutano ya kampeni ambapo bwana Iddi Mwapachu alisema mpakasasa hawajapata malalamilo yeyote pamoja na kuwa wameisha ongea na vyombo vya ulinzi juu ya Makosa ya matumizi ya muda wa mikutano kwa vyama vya siasa.
Mwisho.