Mwakilishi
wa Shirika la Kimataifa la Unicef Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika
sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa Mkoa wa Mbeya15
Octobar 2015
Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu akitoa taarifa ya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mbeya kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa 15 Octobar 2015.
Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700 .
Viongozi
mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakishiriki
kikamilifu tukio la makabidhiano ya magari ya wagonjwa Mkoa wa Mbeya 15
Octobar 2015 kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF.(P.T)
Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya
Kastro Msigala Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za makabidhiano ya magari kumi ya kubebea wagonjwa ambayo yametolewa na shirika la kimataifa la UNICEF Octobar 15 mwaka huu.
Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Kastro Msigala akikata utepe kuashiria kupokea rasmi msaada wa magari hayo kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF msaada ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 700.
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF.
Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya .
Meza Kuu katika picha ya Pamoja na timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Mbeya .
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF.
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia watoto Duniani (UNICEF)
limekabidhi msaada wa magari kumi ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya
shilingi mil 700.7 kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .
Aidha
shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za
afya katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30
pamoja na zahanati 154 sanjali na kuvipatia vifaa muhimu vya kutolea
mafunzo kwa watumishi wake.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Octobar 15 mwaka huu Mwakilishi wa shirika la UNICEF nchini Tanzania
Dkt Jama Gulaid amesema shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi
bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.
Amesema
mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua
wigo kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote
katika kipindi cha miaka miwili .
Aidha
Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na
wanawake wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja
vile vya uchunguzi wa ujauzito ,upasuaji sanjali na vifaa kuwasaidia
watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya utoaji
wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu ICU.
Aidha
amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanaweka juhudi
kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa
kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata huduma za afya
bure kwa wakati.
Awali
akisoma taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto katika mkoa mbeya
mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu
amesema toka shirika hilo la UNICEF lianze kufanya mwaka 2012 huduma za
afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza kuzuia vifo vya
uzazi na vya watoto wachanga.
Amesema
kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa vinatokea katika vituo vya
huduma vimepungua kutoka 140 kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa
mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa
mwaka 2012 hadi kufikia 568 mwaka 2014 ambapo punguzo hilo ni sawa na
asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu
Kastro Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo
sanjali na kutoa wito kwa viongozi wa halmashauri ambao ni wakurugenzi
na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutoa
huduma stahiki kwa wananchi.
Msaada
huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya
ambazo ni Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na
Kyela na Momba .
No comments:
Post a Comment