TASWIRA ZA MKUTANO WA FUNGA KAZI WA CCM JANGWANI - LEKULE

Breaking

24 Oct 2015

TASWIRA ZA MKUTANO WA FUNGA KAZI WA CCM JANGWANI

Mwenyeki wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea Urais wa CCM Dt John Pombe Magufuli,mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani.

Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar es salam na Vitongoji vyake,katika uwanja wa Jangwani

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt Jonhn Pombe akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya jangwani,alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio na hatimae aibuke kinara katika nafasi ya Urais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi Mkuu.
Nyomi uwanja wa Jangwani likiwa tuliiiii.
Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar na viunga vyake wakati wa kufunga kampeni za lala salama za Mgombea Urais wa chama hicho.Dkt Magufuli,uliofanyika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.
Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa wametulia wakisikiliza Sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya viwanja vya Jangwani.
Sehemu ya umati wa watu
Wananchi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakifutilia mkutano wa kampeni wa CCM .
Sehemu ya maelfu ya wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Jangwani kwenye mkutano wa kampeni za lala salama,ambapo Mwenyekiti wa CCM,Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa ndiye mgeni rasmi,wakiwemo vingozi mbalimbali wa cma na Taifa kwa ujumla.
Mwenyeiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu MKuu wa chama hicho cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.Pichani kulia ni  Mke wa Mwenyekiti wa CCM,Mama Salma Kikwete
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth Magufuli ,kwenye mkutano wa kampeni za lala salama uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.
Mzuka umempanda basi kwa raha zake viwanja vya jangwani.

Mfuasi wa CCM katika umakini wa kufautilia yanayojiri kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Jangwani jijini Dar

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Ndugu Kipi Warioba.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Ndugu Jerry Silaa.

No comments: