Wahamiaji wakisubiri kuingia Slovenia, Oktoba 19, 2015,Trnovec.
Na RFI
Slovenia,
moja ya nchi ndogo za Ulaya, inakabiliwa na mgogoro wa wahamiaji, baada
ya kuzidiwa na "wingi" wa maelfu ya wahamiaji wanaotokea katika nchi za
Balkan, huku wengi wao wakionekana wamechoka.
Hayo yanajiri wakati wibi la wahamiaji wanaotafuta hifadhi wameendelea kuelekea Uturuki.
Hali ni
tete na huenda ikaenea katika ncha mbili za barabara zinazotokea katika
nchi za Balkan inayoingia Ulaya Magharibi. Wanaume, wanawake na watoto,
ikiwa ni pamoja na raia wa Syria, Afghanistan na Iraq waliokimbia vita,
wameendelea kuingia katika nchi ya Slovenia. Ugiriki inakabiliwa siku za
hivi karibuni na " wimbi la wahamiaji ," kwa mujibu wa shirika la Umoja
wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (HCR), wakati ambapo Slovenia
ikisema kuzidiwa na wingi wa wahamiaji kwenye mipaka yake.
Serikali
ya Slovenia, ambayo imebaini kwamba wahamiaji 19,500 waliingia katika
ardhi yake tangu Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita, imetoa wito kwa
Umoja wa Ulaya kuisaidia. Slovenia tangu majira ya Joto imekua ikijaribu
kukabiliana na hali hii isiyokuwa ya kawaida lakini inashindwa kupata
ufumbuzi.
Baada ya
Hungary kufunga mpaka wake na Croatia, wahamiaji sasa wanapitia katika
nchi hii ndogo yenye wakazi milioni mbili ambayo imeamua kupanua
madaraka ya jeshi kwa aina ya kipekee.
" Wingi
wa wahamiaji katika siku tatu zilizopita inazidi uwezo wetu ", serikali
imeonya, na kuhakikisha hata hivyo kuwa matumizi ya jeshi " haimanishi
hali ya hatari."
No comments:
Post a Comment