Meneja
Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akizungumza na
waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya
Posta duniani, inayoadhimishwa kesho, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) jijini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Elia Madulesi.
Baadhi
ya waandishi wa habari, wakichukua habari na kumsikiliza Meneja Masoko
wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, wakati akizungumza
nao, jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta
duniani, inayoadhimishwa kesho, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
jijini. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi Mkuu wa TPC, Wilfred Miigo.
Baadhi
ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Meneja Masoko wa Shirika la Posta
Tanzania (TPC), David George, wakati akizungumza nao, jijini Dar es
Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta duniani.
Meneja
Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), David George, akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipokuwa akizungumza nao jijini,
Dar es Salaam jana, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Posta duniani,
inayoadhimishwa leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini.
Na Mwandishi Wetu
UKUAJI
wa Sayansi na Teknolojia ya habari hapa nchini kama mitandao ya simu za
mkononi imeathiri kwa kiasi kikubwa huduma za uandishi wa barua na
kutuma kwa njia ya posta.
Hayo,
yameelezwa Dar es Salaam jana na Meneja Masoko wa Shirika la Posta
Tanzania (TPC), David George kwa niaba ya Kaimu Postamasta Mkuu na
Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Fortunatus Kapinga, alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari jkuhusu Maadhimisho ya Siku ya Posta
Duniani.
Maadhimisho
hayo, yanayofanyika leo duniani kote nchini Tanzania yatafanyika
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), ambapo alisema
kutokana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano uandikaji wa
barua umekuwa ukiathiriwa kwa kiasi kikubwa kwani watu wengi wamekuwa
wakiwasiliana kwa njia ya simu kupitia meseji fupi (SMS).
“Kutokana
na athari hizo, shirika limeamua kuanzisha shindano la uandishi wa
Insha kwa wananfunzi wa Shule za Msingi na Sekondari ambapo washindi 10
wa shindano hilo watapata zawadi mbali mbali, ikiwemo vifaa vya shule
vya kusomea na kujifunzia,”alisema.
Alisema
shindano hilo, limekuwa likiwaongezea wanafunzi hao hamasa ya uandishi
wa barua kwani vijana wengi wa sasa hawajui hata kuandika barua za
kikazi kwani hata maombi ya kazi huangalia kwenye mtandao au kutuma
taarifa kwa njia ya mtandao.
“Katika
uandishi wa isha hizo tuliweka mada ya tueleze juu ya dunia unayopenda
kukulia, yenye kauli mbiu ya ubunifu, utangamano na ushirikishwaji ni
vichocheo muhimu kwa mustakabali wa posta,”alisema.
Ofisa
huyo, alisema kutokana na ubunifu na utengamano na ushirikishwaji
imekuwa ni kichocheo katika kufanikisha malengo ya shirika hilo, ikiwa
ni pamoja na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).
“Tunaendelea
kutekeleza mfumo wa Tehama ujulikanao kama ‘Postal Global’ ambao hadi
sasa ofisi 95 zimeunganishwa ambapo lengo letu ni kuunganisha ‘on line’
ofisi zote ili kuwe na huduma jumuishi za kimtandao,”alisema.
Katika maadhimisho hayo, washindi watatu wa insha watatunukiwa zawadi zao.
Pia
Shirika katika kuadhimisha siku hiyo, alisema kuwa wamekusudia leo
kwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa wa saratani ya shingo ya
kizazi katika Taasisi ya saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment