RATIBA KOMBE LA DUNIA 2018: KUANZA KUTIMUA VUMBI ALHAMISI OKTOBA 8, 2015 LIONEL MESSI, NEYMAR NJE SAFARI YA URUSI IKIANZA! - LEKULE

Breaking

8 Oct 2015

RATIBA KOMBE LA DUNIA 2018: KUANZA KUTIMUA VUMBI ALHAMISI OKTOBA 8, 2015 LIONEL MESSI, NEYMAR NJE SAFARI YA URUSI IKIANZA!

Lionel Messi na Neymar, watakuwa nje wakati Nchi zao Argentina na Brazil zikianza Mechi zao za kwanza za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kusaka nafasi za kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia hapo Alhamisi.
Messi ataikosa Messi ya Argentina na Ecuador kwa vile ni majeruhi wakati Neymar ataikosa Mechi ya Nchi yake Brazil ikicheza Ugenini na Chile zikiwa ni Mechi za kwanza ambazo zitachezwa Alhamisi.
Mbli ya kwamba Mechi hizi ni muhimu kwenye Kundi hili lenye Nchi 10 ambazo 4 za juu ndizo hufuzu moja kwa moja kwenda Finali za Kombe la Dunia, Brazil na Argentina zina deni kwa Washabiki wao baada ya kufanya vibaya kwenye Copa America.
Copa America, Mashindano ya Mataifa ya Nchi za Marekani ya Kusini, yalifanyika Mwezi Juni na Julai Nchini Chile ambapo Wenyeji hao walibeba Kombe baada ya kuwabwaga kwa Mikwaju ya Penati Argentina.

Kwenye Mashindano hayo, Brazil walitolewa kwa Mikwaju ya Penati kwenye Robo Fainali na Paraguay na kabla ya hapo walipata pigo baada ya Kepteni wao Neymar kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na kisha kufungiwa Mechi 4.
Licha ya Brazil kumkosa Neymar kwenye Mechi yao na Chile, Nchi hiyo inarekodi nzuri dhidi ya Mabingwa hao wa Copa America.
Katika Mechi za Mchujo za Kombe la Dunia, Brazil wamefungwa mara moja tu na Chile, 3-0 kwenye Mechi za kuelekea Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2002, na tangu wakati huo wamecheza Mechi 14 na Brazil wameshinda 12 na Sare 2.
Katika Mechi yao ya mwisho kukutana, Kirafiki Mwezi Machi Jijini London, Brazil iliifunga Chile 1-0.

KOMBE LA DUNIA 2018
Marekani ya Kusini-Mechi za Mchujo
Alhamisi Oktoba 8

22:00 Bolivia v Uruguay
23:30 Colombia v Peru
Ijumaa Oktoba 9

00:01 Venezuela v Paraguay
02:30 Chile v Brazil
03:00 Argentina v Ecuador
Jumatano Oktoba 14
00:01 Ecuador v Bolivia
02:00 Uruguay v Colombia
04:00 Brazil v Venezuela
04:00 Paraguay v Argentina
05:15 Peru v Chile