RAIS KIKWETE KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BANDARI YA BAGAMOYO
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete Alhamis Wiki hii anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Mradi
huo wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo utakaokuwa wa aina yake Afrika
Mashariki na Kati, unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu Dk Florens Turuka, Rais Kikwete ataweka jiwe hilo
la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa awamu ya kwanza ya mradi; ambayo ni
ujenzi wa wa bandari hiyo iliyopo wilayani Bagamoyo.
Turuka
alisema, mradi mzima wa ujenzi utajumuisha eneo hekta 800 kwa ajili ya
ujenzi wa bandari na eneo la hekta 1,700 kwa ajili ya ukanda wa viwanda.
Eneo
hilo litaendelezwa chini ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania,
Kampuni ya China ya Merchants Holdings International (CMHI) na Mfuko wa
Taifa wa Dharura wa Oman (SGRF).
Chini
ya ushirikiano huo, Serikali inawakilishwa na Mamlaka ya Bandari ya
Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya
Nje,(EPZA), Oman itawakilishwa na SGRF na China CMHI.
“Pamoja
na bandari na ukanda wa viwanda, mradi huu pia utahusisha ujenzi wa
miundombinu kama vile reli, mitandao ya barabara, umeme, umeme, gesi na
mitandao ya mawasiliano,” alisema Dk Turuka.
Mradi
huo unatarajiwa kuibadili Tanzania na kuwa kituo kikuu cha usafirishaji
kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa ambao wataunganishwa na
viwanda vitakavyozalisha bidhaa zilizoongezewa ubora.
Kwa
mujibu wa Dk Turuka, wazo la kuwepo mradi huo, limetokana na uhusiano
wa muda mrefu wa kidiplomasia baina ya Tanzania, China na Oman katika
kuhamasisha uimarishaji wa viwanda Afrika jambo litakalosaidia kuongeza
ajira nchini.
Kuanzishwa
kwa mradi huo, kuliibuka tangu mwaka 2008, Rais Jakaya Kikwete
alipotembelea China na kuzungumza na Rais wa nchi hiyo, Hu Jintao, na
kuafikiana kujenga bandari hiyo.
Sherehe za kuweka jiwe la msingi zitahudhuriwa na wageni wa kimataifa na wa ndani wakiwemo wawekezaji katika mradi huo.
Wengine
wanoatarajiwa kuhudhuria ni, wana diplomasia na ujumbe kutoka kwa
Sultani wa Oman utakaoongozwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano
nchini humo, Shehe Abdullah Al Saadi.
Ujumbe
kutoka China utaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CMHI ambaye pia ni
Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni ya China Merchant Group Dk Hu
Jianhua.
No comments:
Post a Comment