Meneja
wa Mfuko wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni
wa PSPF, Mwanjaa Sembe, (aliyesimama), akiwaongoza wanachama wapya
waliojiunga na mpango huo, wakati wa warsha ya siku moja
iliyowakutanisha maafisa na mabalozi wa PSPF, na wanakikundi wa Sauti ya
Wanawake Wajasiriamali Tanzania, (VOWET), kwenye ukumbi wa Belmonte
jijini Dar es Salaam, Oktoba 13, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan
Said)
Na K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umezidi k”kupenya’ kwenye sekta binafsi na kuvuna
wanachama zaidi kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari yaani PSS,
ambapo wanakikundi wajasiriamali wa kundi la Sauti ya Wanawake
Wajasiriamali Tanzania (Voice of Women Entrepreneurs Tanzania-VOWET).
Wanachama
hao wapya walijiunga baada ya kushiriki warsha ya siku moja ambayo
ilifanyika kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jingo la makao makuu ya
PSPF, jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2015, ambapo Mabalozi wa Mfuko
huo, Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto na Mwanamitindo wa Kimataifa
anayeishi na kufanyia kazi zake jijini New York Marekani, Flaviana
Matata, walishiriki kutoa “Darasa” kuhusu umuhimu wa Watanzania walio
katika sekta bionafsi kuchangamkia fursa kupitia kuiunga na uamancaha wa
Mfuko huo kupitia mpango wa PSS.
Mabalozi
hao waliongozwa na Meneja wa Mpango wa PSS, Mwanjaa Sembe, na Afisa
Masoko Mwandamizi wa Mfuko huo, Magire Werema, ambao wote kwa pamoja
walifafanua na kueleza kwa kina faida za kuwa mwanachama wa Mfuko huo,
ambapo kwa muda mfupi baada ya kujiunga Mwanachama anawezakufaidi mafao
mbalimbali yatolewayo na Mfuko huo ikiwemo mikopo ya nyumba, Fao la
Elimu, na mengine mengi.
Kufuatia :Darasa” hilo, wanachama wa VOWET walijiunga na Mfuko huo kupitia mpango wa PSS
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mwanjaa Sembe, akitoa mada
Magire Werema, Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF
Balozi wa PSPF, Mwanamitindo wa Kimataifa aishie nchini Marekani, Flaviana Matata
Balozi wa PSPF, Msanii maarufu Tanzania, Mrisho Mpoto akitoa mada
Mjumbe wa Bodi ya Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania, VOWET, Anne A. Ottieno, akiuliza swali
Wanachama
wa VOWET, wakijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari
PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakat wa Warsha hiyo
Mwanachama wa VOWET, akijaza fomu tayari kuwa Mwanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS
Afisa
Masoko Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Rahma J Ngassa,
(kushoto), akiteta jambo wa Balozi wa Mfuko huo, Flaviana Matata
Rahma akiteta jambo na Meneja wa Flaviana Matata, Shamim Mwasha(kulia)
Meneja
wa Mpango wa PS, Mwanjaa Sembe, (kushoto), akimsikiliza Mjumbewa Bodi
ya VOWET, Anne Ottieno wakati akijiandaa kujaza fomu za kujiunga na
Mpango huo
Flaviana (wapili kulia), akiwaelekeza wanachama wa VOWET, jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na Mpango wa PSS
No comments:
Post a Comment