RAIS JAKAYA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA JENGO LA MOROCCO SQUARE JIJINI DAR ES SALAAM - LEKULE

Breaking

8 Oct 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA JENGO LA MOROCCO SQUARE JIJINI DAR ES SALAAM

Rais  Jakaya Kikwete amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), chini ya Mkurugenzi wake Nehemia Mchechu kwa mradi wa ujenzi wa jengo la Moroco Square ambao utagharimu sh.bilioni 150 za kitanzania hadi kukamilika kwake. 
 Mradi wa ujenzi huo utakamilika mwaka 2017 na jengo litakuwa na mita za mraba 110,000 na ukiwa na majengo manne.
Mawili ni kwa ajili ya ofisi , moja hoteli na nyingine nyumba za makazi ya watu 100, ghorofa 20 na kiwanha cha ambapo mawili ni kwa ajili ya ofisi, moja Hoteli na lingine ni kwa ajili ya nyumba za makazi ya watu 100 , ghorofa 20 lenye eneo la kiwanja cha ndege kwa juu yake. 
 Akizungumza Dar es salaam jana, wakati wa uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa eneo hilo jana, Rais Kikwete alisema mradi huo ni mkubwa kuliko yote katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na utaifikisha nchi katika hatua nyingine za kimaendeleo. 
 Aliongeza kuwa ni mambo mapya kuanzishwa Tanzania tofauti na siku za nyuma, hivyo alilipongeza NHC kwa kwenda na wakati. Rais Kikwete alisema utakapokamilika mradi wa eneo hilo la Mororco Square utakuwa na faida nyingi kama kupunguza gharama za wananchi kwenda mijini kutokana na huduma zote za kijamii kupatikana eneo hilo. 
 Alitoa mwito kwa NHC kufungua huduma ya Online ili watu wasipate shida wawe wanafanya kila kitu kupitia mitandao badala ya kuhangaika barabara kwenda kutafuta huduma na matokeo yake wanapoteza muda. 
 Alisema katika kuhakikisha huduma zinafanyika kwa urahisi inabidi ziwekwe barabara za juu ili watu wanaopita katika eneo hilo wavuke salama. 
"Pale Morocco kuna njia nne, hivyo kinachotakiwa ni kuweka barabara ya juu lakini sijui kama itawezekana kutokana na kuwa namaliza muda wangu, lakini nawaahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za NHC, hivyo changamoto zenu zitatatuliwa "alisema. 
 Kwa upande wake, Mchechu alifafanua eneo hilo litakuwa na viwanja vya michezo kwa watoto, maduka hivyo ni kitovu cha kuchangamsha mji kutokana na kuwa lipo katikati ya mji. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Zakhia Meghji alisema anaamini kuwa Rais ajaye ni Dk.John Magufuli, hivyo anaamini ataendeleza mradi huo aliouacha Kikwete. 
Alisema umefika wakati wa kutungwa sheria itakayowezesha wageni kununua nyumba hizo kutokana na iliyopo hairuhusu ili kupanua soko kwa wateja. 
Mradi huo umefanikiwa kwa kupata mkopo wa fedha kutoka Benki ya CRDB chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu, Dk. Charles Kimei. 

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki wakati wa hafla hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakiwa kwenye sherehe hiyo.
 Wadau mbalimbali na Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakiwa kwenye sherehe hiyo.

Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu alipowasili  katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC) Mama Zakia Meghji  alipowasili  katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Irene Isaka  alipowasili  katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akisalimiana na watndaji wa NHC alipowasili  katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam

Sehemu ya mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Taswira ya mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Sehemu ya mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akiongea katika hafla hiyo
Hafla kwenye mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akiongea katika hafla hiyo
Sehemu ya wadau wa mradi huo

Rais Jakaya Kikwete (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC), Zakhia Meghji (kulia) na Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi, William Lukuvi wakipiga makofi kumpongeza Rais Kikwete katika siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika sanjari na hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC), Zakhia Meghji (wa pili kulia), akimkabidhi zawadi ya sherehe yake ya kuzaliwa.

 Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifungua shampeni kumpongeza Rais Kikwete katika siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Rais Kikwete akihutubia katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam

Rais Kikwete akipata maelezo ya  mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akipata maelezo ya  mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam

Wanahabari kazini
Rais Kikwete akipata maelezo ya  mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akipata maelezo ya  mradi wa Jengo la Morocco Square jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Kikwete akifunua pazia kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na naibu wake Mhe Angela Kairuki.
 Vifijo baada ya Rais Jakaya Kikwete akifunua pazia kuashiria  uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Jengo la Morocco Square Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi 
Rais Kikwete akimpongeza  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk.Charles Kimei kwa benki hiyo kutoa mkopo wa kuywezesha mradi huo 
 Picha ya pamoja na watendaji wa NHC na viongozi wa Bodi ya shirika hilo na Dr. Kimei
 Picha ya pamoja na wapangaji waliokwisha chukua sehemu Morocco Square
 Rais Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya TSN Bwana Farouqh ambaye kampuni yake imeshachukua sehemu ya kufungua supermarket
 Rais Kikwete akitembezwa kuona maendeleo ya ujenzi wa Morocco Square
 Rais Kikwete akitembezwa kuona maendeleo ya ujenzi wa Morocco Square
 Rais Kikwete akitembezwa kuona maendeleo ya ujenzi wa Morocco Square
 Baada ya kutoka Morocco Square Rais Kikwete alielekea mtaa wa Mindu ambako alizindua rasmi jengo la NHC la Mindu Place
Rais Kikwete akilakiwa na watendaji wa NHC
 Rais Kikwete akilakiwa na watendaji wa NHC
 Rais Kikwete akilakiwa na watendaji wa NHC
 Rais Kikwete akilakiwa na baadhi ya wananchi walionunua fleti kwenye mjengo huo
 Rais Kikwete akilakiwa na baadhi ya wananchi walionunua fleti kwenye mjengo huo
 Rais Kikwete akilakiwa na baadhi ya wananchi walionunua fleti kwenye mjengo huo
 MC Ephrahim Kibonde akielezea muhtasari wa ratiba
 Sehemu ya wakaazi wa Mindu Place
  Sehemu ya wakaazi wa Mindu Place
  Sehemu ya wakaazi wa Mindu Place
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC), Zakhia Meghji 
 Rais Kikwete akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akiongea kabla ya uzinduzi wa Mindu Place
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akifafanua jambo
 Rais Kikwete akiongea na Mama Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, na  Maendeleo ya Makazi Mhe Angela Kairuki
 Rais Kikwete akiongea na Mama Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, na  Maendeleo ya Makazi Mhe Angela Kairuki na Bw. Mchechu
 Wakaazi wa Mindu Place
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi akitaja majina ya  wakaazi wa Mindu Place ambao wamenunua fleti za hapo.
 Wakili Alex Mgongolwa na mkewe wakipokea hati ya fleti waliyonunua Mindu Place
 Rais Kikwete akimpatia Dkt Twalib Ngoma hadi ya fleti ya Mindu Place
 Familia iliyonunua fleti  Mindu Place ikipokea hati yake ya umiliki
 Mkaazi wa Mindu Place akipokea hati yake kwa furaha
 Wakaazi wa Mindu Place wakifurahia hafla hiyo
 Rais Kikwete akimkabidhi hati ya fleti ya Mindu Place Mhe Nizar Karamagi
 Mkurugenzi Mkuu wa Azania Bank akikabidhi mfano wa hundi kwa mmoja wa wakaazi wa Mindu Place ambao wamepata mkopo kununulia fleti hapo mjengoni
 Mdau mwingine ambaye kapata mkopo toka CRDB wa kununulia fleti
 Rais Kikwete akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua jengo la Mindu Place
 Wadau wakipata kumbukumbu
 Rais Kikwete akifunua pazia kuzindua Mindu Place
 Rais Kikwete akiongea na mmoja ya watoto wanaoishi na familia zao Mindu Place
 Watoto wanampenda Rais Kikwete kama anavyowapenda wao
 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua Mindu Place
 Rais Kikwete akiwa katika fleti ya familia ya Wakili Alex Mgongolwa kujionea fleti za Mindu Place zilivyo
 Rais Kikwete akipokea zawadi ya Birthday toka familia ya Wakili Alex Mgongolwa
 Wakaazi wa Mindu Place wakipata picha za kumbukumbu na Rais Kikwete
  Wakaazi wa Mindu Place wakipata picha za kumbukumbu na Rais Kikwete
 Ni wakati wa picha za kumbukumbu

Rais Kikwete na watoto wa Mindu Place.
PICHA NA IKULU

No comments: