Msimamizi
wa uchaguzi jimbo la Singida mjini, Joseph Mchina (kulia) akimkabidhi
Mwalimu Mussa Ramadhan Sima, cheti cha ushindi wa ubunge jimbo la
Singida mjini leo.
Na Nathaniel Limu, Singida
Mgombea
wa nafasi ya urais kupitia CCM, Dk.John Pombe Magufuli, amezoa kura
36,035 katika jimbo la Singida mjini sawa na asilimia 64.09 za kura zote
56,558 zilizopigwa.
Wagombea
wengine wa nafasi ya urais na kura zao kwenye mabano kuwa ni mgombea wa
Ukawa Lowassa Edward Ngoyai (19,007), mgombea wa ACT Wazalendo Anna
Mghwira (235),Mgombea wa ADC Chief Lutalosa Yemba (87), mgombea wa
CHAUMMA Hashimu Rungwe (64), mgombea wa NRA Kasambala Janken Maliki (10)
na mgombea wa TLP, Lyimo, Macmilian Eliofoo (12).
Akitangaza
matokeo hayo leo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida mjini Joseph
Mchina,alisema kuwa nafasi ya umbuge umechukuliwa na mwalimu Mussa
Ramadhan Sima,ambaye amejizoelea kura 36,690 sawa na asilimia 67 ya kura
56,272 zilizopigwa.
Alitaja
wagombea wengine na kura zo kwenye mabano kuwa ni mgombea wa CHADEMA
(16,702),Mwamvua Haji wa CUF (782) na Jeremia Wandili Act Wazalendo
(763).
“Kwa
ujumla zoezi la uchaguzi limeenda vizuri kama tulivyotarajia na
nawashukuru sana wapiga kura wa jimbo letu la Singida mjini kujitokeza
kwa wingi kushiriki haki yao ya kuchagua viongozi wanaowapenda”,alisema
Mchina.
Mbunge Mteule Musa Sima akiwa hati maalumu ya utambulisho ya kuwa Mbunge wa Singida Mjini.
Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya ACT Wazalendo Jeremia Wandiri (katikati) akimpongeza Musa Sima.
Baadhi
ya wana CCM jimbo la Singida mjini wakisherehekea ushindi wa mwalimu
Mussa Ramadhan Sima baada ya kuwagaragaza wapinzani wanne akiwemo Mgana
Msindai wa CHADEMA.
Mbunge
wa zamani wa viti maalum mkoa wa Singida, Martha Mlata (wa pili kulia)
akijumuika kumpongeza mwalimu Mussa Ramadhan Sima baada ya kuwagaragaza
wapinzani wanne.
Mbunge
mteule wa jimbo la Singida mjini, mwalimu Mussa Ramadhan
Sima,akiwapungia wana CCM na wananchi wa mji wa Singida muda mfupi baada
ya kutangazwa mshindi.
Moja
ya magari yaliyokuwemo kwenye msafara wa mbunge mteule wa CCM jimbo la
Singida mjini Mwalimu Mussa Ramadhan Sima baada ya kutangazwa kunyakua
nafasi hiyo.(Picha na Nathaniel Limu).
No comments:
Post a Comment