Mshindi
wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Kayumba Juma (katika),
akiwa ameshikilia fedha zake muda mfupi baada ya kuibuka kidedea kwenye
fainali hizo zilizokuwa zikifanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi
wa King Solomoni uliopo Namanga jijini Dar es Salaa.
Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Madam Rita (wa pili kutoka kushoto), akimtangaza mshindi huyo.
Washiriki waliongia kwenye 6 bora ya mashindano hayo wakiwa jukwaani kabla ya mchujo huo kuanza
Mmoja
wa Majaji wa shindano hilo (kulia), Master Jay akiingia ukumbini hapo
huku akiwa ameongozana na mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo fleva
Shaa.
Majaji wakiwa kwenye meza yao ya kuratibia mashindano hayo.
Peter Msechu akiwa katika pozi kwenye Red Carpet.
Wasnii wanaounga kundi la Navy Kenzo wakipagawisha jukwaani hapo.
Msanii kutoka nchini Nigeria, Run Town anayetamba na kibao chake cha Gallardo, akipagawisha jukwaani hapo.
Mmoja wa washiriki waliokuwa wakichuana jukwaani hapo, Angel Marykato akisaka milioni 50.
Vijana wanaounda kundi la Yamoto Bendi wakitoa burudani kwenye fainali hizo.
Msanii wa Dansi Christiani Bella akitunza na mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye fainali hizo.
Bosi anayesimamia lebo ya Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella akishuhudia kwa makini fainali hizo.
Mshiriki wa Shindano hilo kutoka Arusha, Frida Amani akipagawisha jukwaani hapo kuwania kitita cha shilingi milioni 50.
Kala Jeremiah akikumbushia enzi zake katika mashindano hayo.
Msanii wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ akiwa katika pozi kwenye red Carpet ya mashindano hayo.
Ben Poul akiwa katika pozi na mmoja wa mashabiki zake.
Baadhi ya washiriki waliyotolewa mapema kwenye kinyang’anyiro hicho wakihojiwa muda mfupi baada ya kuwasili ukumbini hapo.
Msanii wa Filamu, Muna Alphonce akiwa katika ubora wake kwenye tamasha hilo.
Kayumba akitunzwa na mashabiki wake kabla ya kutangazwa kuwa mshindi.
Madam Rita akifuta machozi muda mfupi baada ya kumkabidhi mshindi kitita cha shilingi milioni 50.
Madam Rita akiwa kwenye pozi.
Mmoja ya kikundi cha kudansi kikitumbuiza jukwaani hapo.
Mpiga picha Musa Mateja (kushoto), akihojiwa mara baada ya kuingia ukumbini hapo.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia burudani hizo kwa makini.
Kayumba
Juma wa jijini Dar es Salaam juzi usiku aliibuka mshindi wa shindano la
kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka 2015
baada ya kuwabwaga washiriki wengine watano waliofika hatua ya fainali,
hivyo kutwaa kitita cha Sh50 milioni. Mbali na kuondoka na fedha hizo,
kijana huyo amepewa bima ya afya ya mwaka mzima kutoka kwa kampuni ya
Jubilee Insurance.
Juma
aliibuka kidedea katika fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa King
Solomon Hall, Kinondoni jijini Dar es Salaam zilizopambwa na wasanii
mbalimbali wa muziki.
Mshindi
huyo aliwabwaga washiriki wengine watano ambao walifika hatua ya
fainali; Frida Amani, Nassib Fonabo, Jacqueline Kayengi, Angel Mary Kato
na Kevin Gerson. Licha ya kushindwa kutwaa taji hilo washiriki hao
watano walitoa ushindani mkubwa na kuwapa burudani mashabiki
waliohudhuria kwenye ukumbi huo.
Sambamba
na burudani kutoka kwa washiriki hao, pia wapo baadhi ya wasanii
waliolipamba jukwaa la fainali hizo ikiwa ni pamoja na Kala Jeremiah,
Peter Msechu, Christian bella, Yamato Band pamoja na msanii kutoka
Nigeria, Runtown.
Jaji
kiongozi wa mashindano hayo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Benchmark, Rita Poulsen alimtangaza mshindi huyo baada ya washiriki wote
sita kuchuana jukwaani na kubaki wawili.
Baada
ya wawili hao, Kayumba Juma akiwakilisha Dar es salam na Nassib Fonabo
kutoka Arusha ambao waliingia katika hatua ya mbili bora na kutupa
karata yao ya mwisho kwa kuimba muziki wa mwisho, mashabiki walipiga
kura na muda mfupi baadae Jaji huyo maarufu kwa jina la Madam Rita
alipanda jukwaani na kumtangaza mshindi.
“Mnamjua
mshindi…? Sina maneno mengi maana kazi yangu ni kumtangaza mshindi wa
mashindano ya BSS msimu wa 8 (season eight), mshindi ni.. ni.. Kayumba
Juma’’ alitangaza Madam Ritah huku mashabiki wakishangilia kutokana na
burudani aliyotoa mshindi huyo. Mashindano hayo yanayoandaliwa na
Kampuni ya Benchmark Production 360 yalianza mwaka 2006 kwa kusaka
vipaji vya vijana wa Kitanzania kila mwaka lakini mwaka jana mashindano
hayo hayakufanyika tofauti na ilivyozoeleka.
Baadhi
ya washindi wa BSS kwa miaka tofauti toka shindano lianzishwe ni pamoja
na; Jumanne Iddi, Kala Jeremiah, Peter Msechu, Walter Chilambo na
Emmanuel Msuya.
No comments:
Post a Comment