Mkurugenzi wa Asas Dairies Ltd, Salim Asas Abri (aliyesimama) akitoa maelezo ya kiwanda cha kuzalisha maziwa na bidhaa zake kilichopo mkoani Iringa kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Titus Kamani wakati ya ziara ya kutembelea nyanda za juu kusini kupitia mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Afrika ya Mashariki awamu ya pili.
Mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (East Africa Dairy Development) ni mradi wa miaka mitano (2013-2018) unatekelezwa kwa awamu ya pili katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania kwa mfumo wa kitovu cha maziwa (dairy hub).
Nchini tanzania mradi huu unatekelezwa katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe, ambao unatekelezwa kwa ubia-kongano (consortium partnership) kati yaa Heifer International (msimamizi mkuu wa mradi na kuongoza uzalishaji maziwa) kwa kushirikiana na Techno serve (biashara na masoko ya maziwa).
kiwanda
Mitamba katika shamba la Kibebe linalomilikiwa na Richard Phillips  lillilopo karibu na kijiji cha Tagamenda wilayani Iringa.
Nyati maji (water buffaloes) katika shamba la Asas Dairy Ltd lililopo karibu na kijiji cha Igingilani wilaya ya Iringa Waziri wa maenedeleo ya mifugo pia alitembelea katika ziara yake.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt. Titus Kamani (kushoto) akibalishana mawazo na Afisa mifugo Manispaa ya Iringa Dr. Augustino Nyenza.
Afisa mifugo Manispaa ya Iringa Dr. Augustino Nyenza (wa pili kushoto) akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi machinjio ya kisasa yalipo Ngelewale kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Titus Kamani wakati ya ziara ya kutembelea Nyanda za Juu Kusini (southern highlands) kupitia mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Afrika ya Mashariki awamu ya pili.
Mkurugenzi wa Kibebe Farms Richard Phillips (katikati) akitoa salamu kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt. Titus Kamani wakati ya ziara ya waziri huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa (katikati) Amina Masenza akitoa taarifa ya maendeleo ya sekta ya mifugo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Titus Kamani (wa pili kushoto) wakati ya ziara ya waziri huyo iliyoratibiwa na Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (East Africa Dairy Development). (PICHA ZOTE NA FRIDAY SIMBAYA)