Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako wanawake/akina mama zaidi ya 300 wa manispaa ya Shinyanga wamekutana kujadili namna ya kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu ambao umeukumba mkoa wa Shinyanga.Mkutano huo umeitishwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Akina mama hao waliojitokeza kwa wingi leo jioni Oktoba 06,2015 wameweka mikakati mbalimbali ya kutokemeza ugonjwa kipindupindu ambapo Jana pekee wagonjwa 9 wamelazwa katika kambi maalum jirani na hospital ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambapo kati ya hao 9 wawili wamefariki dunia.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mkutano wake na wanawake zaidi ya 300 katika manispaa ya Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alisema wanawake ni jeshi kubwa na ni walimu wakubwa katika familia hivyo wana nafasi kubwa ya kupambana na kipindu pindu kwa kuimarisha na kuhamasisha usafi kwa akina baba,watoto na hata wanawake wenzao.
"Kipindu pindu ni hatari sana...kinaua lazima tupambane nao kwa nguvu zote..nimewaita ili kila mmoja ajue Shinyanga tuna janga..sasa kila mtu achukue hatua,ugonjwa huu unatokana na uchafu..akina mama mna nafasi kubwa sana katika hili...."alisema Matiro.
Akina mama wakiwa wamenyoosha mikono...kwamba wako tayari kupambana na kipindupindu.....
Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwaeleza akina mama hao kuwa chanzo cha ugonjwa huo ni uchafu yaani kula au kunywa kinyesi cha mtu mwingine hivyo ili kuhakikisha ugonjwa kipindu pindu ni vyema wananchi wakajenga vyoo,kuepuka kunywa maji yasiyochemshwa,kula vyakula vya moto,kuosha matunda kabla ya kula sambamba na kuepuka kunywa pombe za kienyeji.
Afisa afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo alisema ugonjwa huo unazidi kuenea kwa kasi katika manispaa ya Shinyanga ambapo jana pekee wagonjwa 9 walifikishwa katika kambi maalum ya wagonjwa wa kipindu pindu jirani na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Afisa afya huyo alisema ili kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa katika manispaa ya Shinyanga tayari wamepiga marufuku tabia ya akina mama lishe na baba lishe kutembeza vyakula mtaani,unywaji pombe za kienyeji,kuzuia matanga kwenye familia yoyote iliyopatwa na kifo pamoja na kula vyakula kwenye sherehe yoyote.
Afisa afya mkuu wa manispaa ya Shinyanga Elly Nakuzelwa aliwataka wakazi wa Shinyanga kufika haraka hospitali pindi wanapoona dalili za ugonjwa wa kipindupindu ikiwemo kuharisha na kutapika mfululizo.
Mkutano unaendelea
Nakuzelwa aliwataka wananchi kujenga tabia ya kufunika vyoo vya shimo,kuepuka kula vyakula kwenye mikusanyiko ya watu wengi,kuacha kutembeza vyakula mtaani,kuuza vyakula shuleni,kununua mboga zinazouzwa chini badala ya kwenye meza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza juu ya matumizi ya vyoo majumbani kwani chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kipindupindu ni kunywa au kula kinyesi cha mtu mwingine baada ya kuchanganyikana na vyakula ama maji anayokunywa binadamu.
Akina mama kutoka manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini ambapo walikubaliana kuimarisha usafi ili kutokomeza ugonjwa hatari wa kipindupindu
Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa kipindu pindu zilizotajwa ukumbini ni pamoja na kuharisha na kutapika mfululizo.
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Akina mama wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi mbalimbali wa mitaa katika manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa akina mama katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga
Mmoja wa akina mama hao akichangia mawili matatu katika mkutano huo
Katika mkutano huo pia ilibainika kuwa wananchi wengi mjini Shinyanga hawana vyoo hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu
Wanawake hao pia walisisitizwa kujenga tabia ya kuwaelimisha wanaume juu ya umuhimu wa kujenga vyoo
Mkutano unaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumzia kuhusu amani ya nchi ambapo alisema serikali imejipanga vyema kukabiliana na watu waliojiandaa kufanya vurugu ikiwemo kuzuia wanawake na wazee wasipige kura siku ya uchaguzi mkuu nchini utakaofanyika Oktoba 25,2015.
Wanawake hao pia walihamasishana kushiriki uchaguzi mkuu ujao huku wakiiomba serikali kuimarisha ulinzi kwao na wazee kwani kumezuka uvumi kuwa kuna watu watawazuia kushiriki uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akawahamasisha wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kutegemea wanaume...akasisitiza juu ya umuhimu wa kujiunga katika vikundi vya wajasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kwa urahisi zaidi badala ya kufuata mtu mmoja mmoja
Akina mama wakisikiliza kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Maendeleo bila amani ni kazi bure...akina mama wakahamasishana kushiriki kulinda amani ya nchi....
Hakuna kutishana siku ya uchaguzi...mkuu wa wilaya ya Shinyanga akawahakikishia ulinzi siku ya uchaguzi huku akiwataka kulinda kadi zao za kupigia kura.
Wanawake na maendeleo ndiyo makubaliano waliyoafikiana.....
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Afisa mtendaji kata ya Shinyanga Mjini Mathias Masalu akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa mtaa wa Kaunda Joha Mussa akifunga mkutano huo
Akina mama wakitawanyika baada ya mkutano
Kila mmoja na njia yake...kushoto ni Mama Steve na Marietha William wakirudi kwao