Mkuu wa tume ya
uchaguzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amejiuzulu, na hivyo kuzusha shaka
kama uchaguzi wa juma lijalo utafanywa kama ulivyopangwa.
Dieudonne Kombo Yaya,alisema alijiuzulu kwa sababu ya chagizo, kutoka kwa rais na jamii ya kimataifa.Uchaguzi mkuu umeahirishwa mara mbili, kwa sababu za usalama.
Watu kadha wameuwawa katika ghasia zilizozidi hivi karibuni,huku malaki wakihama makwao.
No comments:
Post a Comment