Meneja
wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin (wa pili kushoto),
akiwaonyesha Watafiti kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojkia na wageni kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea, mitambo mipya ya
kuzalisha bia, walipotembelea kiwanda hicho, Dar es Salaam jana
kujifunza kuhusu uendeshaji na aina ya mitambo.
Maofisa
kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wageni wao
kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea wakimsikiliza kwa makini, Meneja wa
Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw Calvin Martin )wa pili
kulia), walipofika kiwandani hapo Dar es Salaam jana kujifunza kuhusu
uendeshaji wa kiwanda, aina ya mitambo na ushirikiano na taasisi
zingine. Kulia ni Meneja Usalama wa TBL, Bw. Renatus Nyanda.
Maofisa wa TBL, Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia na Sayansi wakiwa katika picha ya pamoja
Mkuu
wa Kitengo cha Utafiti Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Rafael Kibunda (kulia), Mtafiti kutoka Wizara hiyo, Profesa
Rogers Msuya (kushoto) na Maofisa kutoka Taasisi ya STEPI ya Korea,
wakimsikiliza kwa makini, Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), Bw. Calvin Martin, walipotembelea kiwanda hicho Dar es Salaam
jana kwa ajili ya kujifunza kuhusu uendeshaji wa mitambo. (Na Mpigapicha
Wetu)
Meneja
wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Calvin Martin
(aliyenyoosha mikono), akifafanua jambo, wakati akiwatembeza maofisa
kutoka WIzara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mkuu wa Kitengo cha
Utafiti, Profesa Rafael Kibunda (wa pili kushoto), Mtafiti Profesa
Rogers Msuya (Kulia) na Profesa Hyunho Kim (kushoto), kutoka Taasisi ya
STEPI ya Korea.
No comments:
Post a Comment