MAKAMU WA RAIS WA MALDIVES AKAMATWA - LEKULE

Breaking

25 Oct 2015

MAKAMU WA RAIS WA MALDIVES AKAMATWA



Makamu wa Rais wa Maldives, Ahmed Adeeb leo amekamatwa akituhumiwa kutaka kumuua rais wake, Abdulla Yameen.
MAKAMU wa Rais wa Maldives, Ahmed Adeeb leo amekamatwa akituhumiwa kutaka kumuua rais wake, Abdulla Yameen.
Ahmed Adeeb anazuiliwa na  atashtakiwa kwa uhaini, Umar Naseer amesema kupitia Twitter.

Rais  wa Maldives,  Abdulla Yameen alimesurika kifo katika boti aliyokuwa akitumia kusafiri.
Rais Abdulla Yameen alinusurika kifo baada ya boti aliyokuwa akitumia kusafiri hadi mji mkuu akitoka kuhiji Mecca mwezi jana kulipuliwa.
Misukosuko ya kisiasa imekuwa ikiyumbisha Maldives miaka ya hivi majuzi.
Mzozo ulizuka baada ya Yameen kushinda uchaguzi, wapinzani wakisema kulikuwa na udanganyifu.
Maafisa wakuu wa polisi walifutwa kazi kutokana na uchunguzi wa mlipuko huo, wiki moja baada ya rais huyo kumfuta kazi waziri wake wa ulinzi.
Polisi wamethibitisha kwamba walimkamata Bw Adeeb akiwa uwanja wa ndege baada yake kurejea kutoka safari ng’ambo.
Bw Yameen hakuumia kwenye shambulio hilo la Septemba 28, lakini mkewe, msaidizi mmoja na mlinzi walijeruhiwa.

No comments: