Kamishna
wa NCCR-Mageuzi wa Mkoa wa Ruvuma, Mchatta Eric Mchatta (kushoto) akiwa
na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, Leticia Ghatti Mosore,
na mwakilishi wa NCCR-Mageuzi, Hamlyn Erasto.
Leticia Mosore (katikati) akisoma taarifa yake.
Wanahabari wakichukua matukio katika hafla hiyo.
Mkutano ukiendelea.
MAKAMU Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR-Mageuzi Tanzania Bara, Leticia Ghatti Mosore,
aliyesimamishwa na Mwenyekiti wake James Mbatia amesema hakuridhishwa na
utaratibu uliotumika kumwajibisha.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar, Mosore amesema kuwa Mbatia amemfukuza
bila kufuata Katiba ya Chama ambayo kupitia ibara ya 27 (3) kifungu (C)
inasema kuwa makamu mwenyekiti ataweza kuondolewa kwa mapendekezo ya
halmashauri kuu ya taifa ya chama hicho kwa kura zaidi ya nusu za
wajumbe halali.
Amefafamua
kuwa Mbatia katika utetezi wake alidai kufuata kanuni hiyo kupitia
kikao cha maadili walichokaa Septemba 22 mwaka huu ambacho alisema
hakikuwa halali kwa kuwa kiliundwa na watu wachache wenye uhusiano wa
kifamilia na undugu na Mbatia.
“Hata
kama kikao hicho kingekuwa kikao halali bado kingekiuka haki ya msingi
ya binadamu ya kupewa muda wa kujitetea, isitoshe kanuni za chama
zinafafanua vizuri kwamba lazima mtuhumiwa apewe majuma mawili ya
kujitetea kimaandishi ambayo mimi makamu mwenyekiti sikupewa,”alisema
Leticia.
Aidha
amesema kuwa taarifa za kufukuzwa kwake alizipata kupitia magazetini
Oktoba Mosi mwaka huu ambapo sababu kuu za kufukuzwa kwake zilitajwa
kuwa anatumika kukihujumu chama kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupanga njama za kumdhuru mwenyekiti
wake.
Leticia
amekanusha madai hayo na kumtaka Mbatia athibitishe kwa kuwataja
viongozi wa CCM anaoshirikiana na akazidi kusimamia kauli yake aliyoitoa
kabla ya kusimamishwa kwamba haridhishwi na mwenendo wa ushirikiano wa
vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa NCCR-Mageuzi
kupewa majimbo 12 tu ambapo sita tayari yamekwishaingiliwa na CHADEMA
hivyo uwezekano wa kushinda kwenye majimbo hayo ni mdogo kwa kuwa kura
zitagawanyika.
No comments:
Post a Comment