Mchezaji wa zamani
wa mpira wa vikapu katika ligi ya NBA nchini Marekani Lamar Odom
hatimaye amepata fahamu siku tatu baada kuzirai ndani ya danguro katika
jimbo la Nevada.
Msemaji amesema kuwa bwana Odom alizungumza na kutoa maamkuzi ya kidole katika kitanda chake cha hospitalini.Alikuwa katika mashine ya usaidizi baada ya kupatikana siku ya jumanne akitokwa na damu puani na mdomoni.
Odom aliwahi kushinda taji la ubingwa akiichezea Los Angeles Lakers.


No comments:
Post a Comment