George
Aloyce Kimaryo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na shtaka la kusambaza taarifa zauongo kupitia katika kundi
la Adios la mtandao wa WhatsApp kuwa Mwanafunzi wa Chuo cha DIT,
Benedict Angello Ngonyani amejitokeza kwa mara ya pili mahakamani na
kuishangaza kwa kumtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Mwamunyange ajitokeze na kukanusha kuwa amelishwa sumu.
Wakili
wa Serikali Jacquline Nyantori akishirikiana na Wakili Mwandamizi wa
TCRA, Johannes Kalungula walidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba kuwa Oktoba 13,2015 katika mtandao huo wa kijamii mshtakiwa huyo
alisambaza taarifa hiyo kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya
Mtandao namba 14 ya 2015.
Baada
ya kusomewa shitaka hilo, mshtakiwa huyo alikana na upande wa mashtaka
ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na Hakimu Simba aliiahirisha
kesi hiyo hadi Novemba 3, 2015 kwa ajili ya kutajwa na kufikiria juu ya
maombi ya dhamana.
Mwanafunzi
huyo wa Chuo cha DIT, Benedict Angello Ngonyani yeye anakabiliwa
na kesi ya kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa WhatsApp na
Facebook kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange
amelishwa sumu.
Tangu
afikishwe mahakamani hapo kwa mara ya kwanza siku 14 zilizopita leo
yaani jana ndiyo alipanda kwa mara ya pili kizimbani mbele ya Hakimu
Respicius Mwijage ambapo Wakili Nyantori alidai kuwa kesi ilikuja kwa
ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.
Nyantori
alidai katika kesi hiyo, kuwa kesi hiyo inahusisha mtandao bado
wanakusanya taarifa ambazo ni za muhimu kupitia mfumo huo.
Hata
hivyo wakili wa kujitegemea, Mnyela Abdallah alijitokeza mahakamani
hapo na kujitambulisha kuwa yeye atakuwa wakili wa mshtakiwa huyo
atakayemtetea kwenye kesi hiyo na akajulishwa kuwa mteja wake amewekewa
zuio la dhamana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Hakimu
Mwijage aliuambia upande wa mashtaka kuwa uliweka zuio hilo la dhamana
na kutoa sababu ndani ya siku hizo 14 na kuwaambia kuwa sasa kuna
umuhimu wa kulijadili dhamana ya mshtakiwa huyo na kitu ambacho
kinapelekea andelee kuzuiwa kwa dhamana yake maana lazima kuwepo na
sababu hivyo aliwataka Novemba 3,2015 kesi itakapotajwa kwa ajili ya
kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la, waeleze sababu.
Ngonyani
amekuwa ni mshitakiwa wa kwanza kufikishwa mahakamani na kufunguliwa
mashtaka kupitia sheria hiyo mpya ya mtandao ambayo inazuia mtu yoyote
kusambaza ama kuchapisha data, taarifa za uongo, uzushi na zile ambazo
hazijathibitishwa ama hazina chanzo pamoja na picha za matusi katika
mitandao ya kijamii.
Katika
kesi hiyo, Ngonyani anadaiwa kuwa Septemba 25,2015, jijini Dar es
Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya WhatsApp na
Facebook kuwa Jenerali Mwamunyange amelishwa sumu na kwamba amepelekwa
Nairobi Kenya kwa matibabu wakati akijua taarifa hizo zilikuwa na lengo
la kupotosha umma.
Mbali
na kesi hiyo, Mshtakiwa Raia wa China, Royce Lee na raia wa Pakistani
Iqbal Wasif na Mohamed Jamil wamepandishwa kizimbani mahakamani hapo
wakikabiliwa na kesi tofauti za kuingiza mitambo ya kielektroniki ya
mawasiliano nchini bila ya kuwa na leseni kutoka TCRA, wakaisimika na
kutoa huduma za simu za Kimataifa kinyume cha sheria na kuisababishia
mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh 500 milioni.
No comments:
Post a Comment