Kampeni
ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa
baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika imeingia Tanzania Octoba
17 kwa waendesha baiskeli 21 kutoka Tanzania kuwapokea wenzao kutoka
Malawi.
Kampeni
hiyo ambayo imeanzia Msumbiji, Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe,
Zambia, Malawi na hatimaye Tanzania na itatia nanga Kenya mapema mwezi
novemba mwaka huu.
Msafara
huo wa waendesha baiskeli kwa Tanzania umeanzia kwenye mpaka wa
Tanzania na Malawi wa Kasumulu ambapo unataratia kwenda mpaka Namanga
watakapoukabidhi kwa waendesha baiskeli wa Kenya.
Kwa
mujibu wa Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina
Mosha lengo la msafara huo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya mabadiliko
ya tabianchi kwa kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini nchini.
Anasema
msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za wananchi ili kuweka
imani zao kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa
kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika Desemba mwaka
huu huko Paris, Ufaransa.
Mama
Mosha anasema kuwa wameamua kutumia uendeshaji wa baiskeli kama njia ya
kuhamasisha jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa sababu chombo
hicho ni rafiki wa mazingira na hakichangii uzalishaji wa hewa ukaa.
Picha zote na tabianchi blog
Waendesha
baiskeli kutoka Malawi wakiwasili kwenye mpaka wa Tanzania na nchi hiyo
tayari kwa kukabidhi kijiti cha kampeni hiyo kwa wenzao wa Tanzania.
Mmoja wa waendesha baiskeli Tanzania ambaye pia ni Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Tanzania, Gilbert Mworia.
Meneja
Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha akizungumza
jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya
tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli.
Waendesha baiskeli wa Tanzania wakiwa katika mji wa Kyela Mbeya
Mama Mosha akiwa na baadhi ya waendesha baiskeli wa Tanzania
Balozi
wa kampeni ya We Have Faith nchini Malawi, Father George Buleya
(kushoto) akiwa na Mratibu wa Vijana kutoka YouthCAN Tanzania, Francisca
Damian wakati wa hafla ya kukabidhiana kampeni hiyo iliyofanyika kwenye
mji wa Kasumulu, Mbeya.
No comments:
Post a Comment