Imelda mtema-GPL
STAA wa
sinema za Kibongo, Kajala Masanja, amefunguka kuwa anamshukuru Mungu
uchaguzi umefika kitu ambacho alikuwa akikiomba usiku na mchana.
Akizungumza
na gazeti hili, Kajala alisema katika kipindi chote cha vuguvugu la
uchaguzi kuna vitu vingi vililala kutokana na kila mmoja
macho,masikio,akili na hata mawazo vilikuwa ni uchaguzi hivyo kushindwa
kufanya chochote.
“Namshukuru
Mungu huu uchaguzi umefika maana ilikuwa ni majanga makubwa hakuna kitu
ulichokuwa unaweza kufanya katika kipindi chote cha kampeni jamani ila
nachoomba zaidi ni amani,” alisema Kajala.Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge
na madiwani nchi nzima unatarajiwa kufanyika kesho.
No comments:
Post a Comment