Zikiwa zimebaki siku 5 kabla ya Oktoba 25, siku ambayo watanzania wataandika historia ya kuiweka madarakani serikali mpya ya awamu ya Tano, kada mwingine Mkongwe wa Chama hicho, ametangaza rasmi kujiweka kando.
Dkt. Eve Sinare, ambaye ni wakili wa kujitegemea aliyekuwa sehemu ya harakati za CCM, alitangaza jana kukihama chama hicho akidai kuwa kimepoteza sifa za utawala bora na kimeshindwa kuwahudumiwa wananchi kwa kuwapa elimu bora iliyotarajiwa.
Dkt. Eve Sinare aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA). Pia, ni Mwenyekiti Mtendaji wa Rex Attoneys na aliwahi kuteuliwa kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Bodi ya Huduma ya Dunia iliyoko Texas inayofahamika kwa jina la World Services Group (WSG).
Hata hivyo, kama alivyosema Balozi Juma Mwapachu wakati anahama chama hicho, Dkt. Eve Sinare ameeleza kuwa hatajiunga na chama chochote cha siasa.
No comments:
Post a Comment