CREATOR: gd-jpeg v1.0 (using IJG JPEG v62), quality = 100
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Francis M. Mwakapalila (pichani) kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali kuanzia juzi, Alhamisi, Oktoba 1 , 2015.
Ndugu Mwakapalila anachukua nafasi ya Bibi Mwanaidi Mtanda ambaye amestaafu kazi kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi wake kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali, Ndugu Mwakapalila alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
03 Oktoba, 2015