Wanafunzi
wasajiliwa jeshini DRCWanaharakati wanaonya kuwa shule huko Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo -DRC, zinatumika kuwaandikisha watoto ili kuingia
jeshini.
Kundi la
kutetea haki za binadamu lenye makao yake makuu nchini Marekani Human
Rights Watch, linasema kuwa makundi yenye silaha yamekuwa yakiwateka
wanafunzi wa katika majimbo ya Kivu ya kaskazini na kusini.
Katika
ripoti yake, kundi hilo pia linayalaumu makundi ya waasi na jeshi la
serikali ya Congo, kwa kutumia shule kama kambi zake za kijeshi au
kuhifadhia silaha.
Katika
ripoti yake, kundi hilo pia linayalaumu makundi ya waasi na jeshi la
serikali ya Congo, kwa kutumia shule kama kambi zake za kijeshiHuman
Rights Watch imeitaka serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
ifanye jitihada zaidi ilikuwalinda watoto.
Mwaka wa
2013 Umoja wa mataifa uliwapatanisha serikali na makundi ya wapiganaji
katika jitihada za kuleta amani na kukomesha uasi uliokuwa ukiendeshwa
na kundi la M23.
No comments:
Post a Comment