Full Time ya Tanzania Prisons Vs Simba October 21 - LEKULE

Breaking

21 Oct 2015

Full Time ya Tanzania Prisons Vs Simba October 21

Klabu ya Simba ambayo Jumamosi October 17 ilicheza na klabu ya Mbeya City ya jijiniMbeya katika mchezo ambao Simba hawakuwa na rekodi nzuri dhidi ya Mbeya Citykwani ilikuwa haijawahi kushinda dhidi ya Mbeya City katika dimba la Sokoine jijiniMbeya.
October 21 ilikuwa ni zamu ya wapinzani wa Mbeya City kutoka jiji moja Tanzania Prisons kuikaribisha Simba katika uwanja wa Sokoine kwani ilikuwa tayari imeshavuna point tatu kutoka kwa Mbeya City siku ya Jumamosi ya October 17. Simba ambao waliingia uwanjani wakiwa na hali ya kusaka ushindi wameshindwa kutamba mbele yaPrisons kwa kukubali kichapo cha goli 1-0.
Klabu ya Simba imekubali kupokea kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Tanzania Prisons, goli la Prisons lilifungwa na Mkopi dakika ya 60. Kwa mara nyingine tena Simba imeshindwa kuondoka na point tatu muhimu kutoka jijini Mbeya licha ya kuwa walifanikiwa kuvunja mwiko wa kutopata matokeo mazuri mbele ya Mbeya City.

No comments: