dar coca 1
Ma Dj walikuwa wakifanya mambo kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri.
-Mamia waburudika Coke Party mikoa ya Dar, Mwanza, Mbeya na Arusha
Onyesho la muziki la Coke Studio ambalo linajumuisha Kolabo ya wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wan je limeanza kurushwa nchini Jumamosi nchini kupitia luninga ya Clouds ikiwajumuisha wanamuziki Ally Kiba,Vanessa Mdee, Ben Pol na Fid Q ambao wanashirikiana na wanamuziki Wangechi,Maurice Kirya,Victoria Kimani na 2Face.
Baada ya uzinduzi huo zilifanyika party za kukata na shoka katika viwanja vya maraha sehemu mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya na Arusha zilzowajumuisha vijana kucheza muziki,kuimba na kufurahi na kujishindia zawadi mbalimbali za Coca Cola.
Mwanza 3
Vijana wakishiriki kuimba Coke Studio Party mkoani Mwanza.
dar coke 5
Ilikuwa ni burudani kubwa vijana wakicheza muziki kwa furaha ndani ya Maisha Club.
dar coke 4
Baadhi ya mayanki waliohudhuria Coke Studio Party wakiwa kwenye picha ya pamoja katika ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.
dar coka 6
Coke Studio Party ulikuwa mjumuiko ulioleta furaha kwa wengi kama inavyoonekana katika kiwanja cha Maisha Club.
mwanza 6
DJ akinogesha mambo ya Coke Studio mjini Mwanza.
mwanza 9
Watu wa rika mbalimbali walifika Coke Studio Party kupata burudani kama wanavyoonekana baadhi yao pichani mjini Mwanza.
User comments
Zawadi mbalimbali zilitolewa katika Party ya Mwanza kama anavyoonekana Masai akijichukulia zawadi katika party ya Mwanza.