Kada wa chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe jana aliwasili kwa chopa kwenye mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha DP Mchungaji Christopher Mtikila.
Wakati
chopa hiyo inatua katika eneo la Msiba wananchi waliacha kusikiliza
Salam mbali mbali za viongozi na kukimbilia kutazama ili kufahamu ni
nani aliyekuwemo ndipo alipoteremka Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe.
Mazishi
ya Mchungaji Mtikila yalihudhuriwa na viongozi kadhaa wa serikalini
akiwemo Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mutungi, mkuu wa mkoa wa
Njombe Dr. Rehema Nchimbi ,wanasiasa pamoja na ndugu na jamaa kutoka
sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Akizungumza
katika mazishi hayo Filikunjombe alisema mbali ya ukorofi wa Mtikila
kwa kile alichokiamini ila kwake alikuwa ni mshauri mkubwa wa Ubunge
wake katika jimbo la Ludewa.
Filikunjombe
alisema katika kuamini kwake na kusimamia anachokiamini hadi umauti
unamkuta alikuwa akitetea kuwepo kwa nchi ya Tanganyika na ndio maana
kazikwa na bendera ya Tanganyika na kudai kuwa hakuna kosa kupigania
Tanganyika kwani Tanganyika inahitajika.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi alisema kuwa Mkoa wa Njombe
umepoteza kiongozi makini na kuwa katika kumuenzi ni vema kwa vyama vya
siasa kuendesha kampeni za amani na utulivu kuwa hivisasa taifa
linaelekea katika uchaguzi mkuu.
Kwa
upande mwingine Naibu Katibu mkuu wa DP Taifa Abdul Mluya alisema kuwa
suala la kifo cha mwenyekiti wake ni utata mtupu na bado wanaendelea
kuchunguza.
Filikunjombe akitoa salamu zake wakati wa mazishi ya Mtikila
Mkuu wa mkoa
wa Njombe Dr Rehema Nchimbi kulia akiwa na Deo Filikunjombe mgombea
ubunge jimbo la Ludewa na mbunge aliyemaliza muda wake, katikati kushoto
ni msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi jana wakati
wa mazishi ya Mchungaji Mtikila
Mjane wa Mtikila akiweka shada la maua
No comments:
Post a Comment