Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma kimesema kuwa kimejipanga kuhakikisha wananchi ambao sio wakazi wa maeneo husika mkoani humo hawashiriki kuwachagua viongozi wasiowahusu.
Katibu
Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Othman Dunga aliyasema hayo hivi
karibuni alipoongea na waandishi wa habari mkoani humo, ambapo alieleza
kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliojiandikisha katika mkoa huo
lakini hawaishi maeneo hayo hawataruhusiwa kupiga kura kuwachagua
wabunge na madiwani.
“Zipo
taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Ukawa wameanzisha utaratibu
wa kukodi magari kwa ajili ya kuwaleta wanafunzi ambao wamejiandisha
hapa kwa ajili ya kupiga kura. Huu ni ushahidi tosha kwamba sio wakazi
wa Dodoma,” alisema Dunga.
“CCM
tumejipanga kuhakikisha hawapigi kura za kiongozi asiyewahusu, mawakala
wetu watakabidhiwa orodha ya wakazi na wataisimamia hiyo,” Dunga ananukuliwa.
Kulikuwepo
na taarifa zisizo rasmi kuwa kuna ‘wasamalia wema’ ambao wamejitolea
kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha katika daftari la
wapiga kura wakati wakiwa vyuoni na sasa wako majumbani, wanarudi katika
maeneo waliyoandikishwa ili wapige kura.
Kwa mujibu wa Dunga, huenda wanafunzi hao wakaambulia kupiga kura kumchagua rais pekee katika eneo walilojiandikishia walipokuwa wanasoma vyuoni hapo.
Kwa mujibu wa Dunga, huenda wanafunzi hao wakaambulia kupiga kura kumchagua rais pekee katika eneo walilojiandikishia walipokuwa wanasoma vyuoni hapo.
No comments:
Post a Comment