Mkazi wa Airport (Paschal Luambano) akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ukonga na Chanika Tesha Stanslaus wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani
*************
Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani imeendelea kuzifikia baa mbalimbali jijini Dar na mikoani ambapo kwa mara nyingine tena promosheni hiyo imekuja kitofauti zaidi kwa wiki hii baada ya kuzifikia baa zaidi ya nne za jijini Dar es salaam.
Baadhi ya baa zilizoshiriki kwenye promosheni hiyo kwa wiki hii ni pamoja na:-Airtel, Serengeti, Blue Sky na Smart zote za Banana-Ukonga jijini Dar es salaam.
Promosheni hiyo ilianza kutimua vumbi kwenye viwanja hivyo kuanzia mida ya saa kumi jioni ambapo kama ilivyo ada burudani ya muziki ilisimamiwa vilivyo na MaDjs na washereheshaji kutoka redio E-fm ambao ni wadau wa Kampeni hii tokea kuanzishwa kwake.
Baadhi ya wateja waliojipatia zawadi mbalimbali kama fulana na bia za bure wakati wa promosheni hiyo mmoja wao ni Paul Ndenjemba (49) ambaye alifunguka na kusema kuwa ameanza kuitumia bia ya Tusker tangu mwaka 1995 na hajawahi kufikiria kuiacha bia hiyo kwa kuwa haimchoshi na akiamka asubuhi anawahi kwenye shughuli zake kama kawaida.
Aliupongeza uongozi mzima wa bia ya Tusker na kusema promosheni kama hizi zinawaleta wateja karibu na kuwafanya wajione wenye fahari kutokana na uwepo wa bia inayowajali wateja wake.
Kwa upande wake Meneja masoko wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella alisema “Sherehe za baa zilizo kwenye mkondo mmoja huiwezesha promosheni hii ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani kuzifikia baa nyingi zaidi na wateja wengi zaidi ambapo pia tunatoa zawadi nyingi zaidi kwa wateja wetu tukiwashukuru na kusema asante kwa kuwa pamoja na bia ya Tusker muda wote”.
Alisema tunafanya haya yote ili kuhakikisha kuwa tunaipa promosheni yetu ya Tusker Fanya Kweli Kiwanjani muonekano wa tofauti kidogo ili wateja wetu wazidi kuburudika na kuhamasika kutokana na ubunifu wetu”.
Aliongeza kuwa pamoja na kuwahamasisha watu kufikia malengo yao, sherehe hizi pia zinabeba ujumbe muhimu wa ubunifu katika kazi na jitihada katika maisha ili kuweza kuzifikia ndoto za maisha yetu.
Hii ni mara ya pili kwa promosheni hii ya Tusker kufanya sherehe za baa zilizo kwenye mkondo mmoja baada ya ile ya kwanza iliyofanyika Sinza Legho ambayo ilizikutanisha baa zaidi ya sita za eneo hilo zikiwemo:-Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.
Tusker Lager pia inayofuraha kuwapongeza washindi waliopo nje ya mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki katika promosheni hii ya Fanya Kweli Kiwanjani kwa wiki iliyopita, miongoni mwa baa hizo ni; - Geneva of Africa (Mrombo) na CR Pub (Moshono)-Arusha, Safari Pub ya Boma-Moshi, Cross Park (Igoma) na Kilimanjaro Pub (Nyegezi)-Mwanza.
KUHUSU BIA YA TUSKER
Bia ya Tusker inazalishwa na Kampuni ya bia ya Serengeti ni bia bora na fahari ya kiafrika yenye zaidi ya miaka 90 ya upishi makini wa bia bora. Bia hii ina asilimia 4.2 ya kilevi na muonekano wake ni katika chupa (kubwa) yenye ujazo wa mililita 500 na (ndogo) yenye ujazo wa mililita 330 zenye rangi ya kahawia.
KUHUSU KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI
Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) inashughulika na huandaaji, uzalishaji na uuzaji wa vinywaji vilivyotengenezwa na shairi, ngano na mtama. Makao makuu ya Kampuni hii Chang’ombe jijini Dar es Salaam, Tanzania na baadhi ya vinywaji vinavyotengenezwa na Kampuni hii ni kama:- Serengeti Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick na Guinness®.
SBL pia husambaza vinywaji mbalimbali vikali vya kimataifa kama Smirnoff Vodka®, Johnnie Walker®, Bailey’s Irish Cream ®, Richot®, Bond 7 Whiskey® and Gilbeys Gin®.
No comments:
Post a Comment