Akina mama wajasiriamali kutoka Wilayani Rorya ambapo kulia ni bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na bi.Magreth Steven.
Akinamama
wajasiriamali katika Kijiji cha Sota, Kata ya Tai iliyopo Wilaya ya
Rorya Mkoani Mara, wamewaomba wagombea watakaobahatika kuingia
madarakani katika uongozi wa awamu ijayo, kuwakumbuka kwa kuwawezesha
mitaji yenye riba na mashariti nafuu ili kuendeleza shughuli zao.
Walitoa
ombi hilo wakati wakizungumza na Mtandao wa BMG (Binagi Media Group),
uliowatembelea hivi karibuni ili kujionea shughuli mbalimbali za
uzalishaji mali pamoja na utunzaji wa mazingira zinazofanywa na wananchi
katika ukanda wa Ziwa Victoria Wilayani humo.
“Sisi
shughuli tunayoitegemea ni hii tu ya kuuza dagaa. Tunawafuata mwaloni
(Mwalo wa Sota) na kuwaleta hapa (Mwamba dagaa) na kuwauza kwa watu
wengine kutoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo nje ya Wilaya hii
(Rorya) kwa ajili ya kwenda kutumia. Alisema bi.Winfrida Joseph ambae ni
mmoja wa akina mama wajasiriamali zaidi ya 20 wanafanya shughuli zao za
kuuza daa katika eneo la Mwamba daa na kuongeza;
“Kiukweli
sisi hapa tuna changamoto ya ukosefu wa mitaji ya uhakika. Hivyo sisi
ombi letu kwa hawa wagombea iwe diwani, mbunge au rais, yeyote yule
atakaechaguliwa kuwa kiongozi, tunaomba atukumbuke. Atusaidie mitaji au
kutuunganisha na taasisi zinazotoa mitaji yenye riba na masharti nafuu
kwani masharti ya haya mabenki mengine yametushinda jamani”
Akinamama
wengine akiwemo bi.Magreth Steven waliongeza kuwa wanaomba kuwepo kwa
soko la dagaa la uhakika kama ilivyo kwa samaki katika mwalo huo wa Sota
jambo litakalowasaidia kufanya biashara zao vizuri zaidi kwa kuwa
hawana msaada mwingine zaidi ya kujishughulisha na biashara hiyo ambayo
inawawezesha kupata mahitaji yao mhimu ikiwemo chakula pamoja na
kuwasomesha watoto wao.
Wananchi
wa Wilaya ya Rorya ambayo asilimia kubwa imetawaliwa na ukame kwa
vipindi virefu vya mwaka, wanategemea zaidi shughuli za uvuvi
ikilinganishwa na shughuli nyingine kama vile kilimo na uvuvi.
Kushoto ni Mjasiriamali kutoka Wilayani Rorya, bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na Mteja wake b.Luise Binagi
Kushoto ni Mjasiriamali kutoka Wilayani Rorya, Bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na Mteja wake b.Luise Binagi.
No comments:
Post a Comment