Afisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Ezra
Ndangoya akimwelekeza sehemu ya kuweka sahihi Bw. Sironga Lowassa
(kulia) ambaye ni mwombaji wa mkopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 katika
ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Septemba 2, 2015).
HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za wanafunzi waliokosea
kujaza fomu zao za maombi. (Picha na Eline Maronga-HESLB)
Afisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Zahra Kitara
(kushoto) akipokea viambatanisho vya maombi ya mkopo kutoka kwa Bw.
Paul Yahhi (kulia) mwombaji wa mkopo ambaye fomu yake ya maombi
ilikosekana baadhi ya viambatanisho jijini Dar es Salaam leo (Jumatano,
Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha taarifa za
wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi. (Picha na Eline
Maronga-HESLB).
Maafisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) (kulia)
wakiwahudumia waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao
fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu jijini Dar es Salaam leo
(Jumatano, Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha
taarifa za wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi.
Afisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Bi. Christina
Chacha (kulia) akimwelekeza jambo mwombaji wa mkopo ambaye fomu yake ya
maombi ilikosekana baadhi ya viambatanisho jijini Dar es Salaam leo
(Jumatano, Septemba 2, 2015). HESLB inaendelea na kazi ya kurekebisha
taarifa za wanafunzi waliokosea kujaza fomu zao za maombi.
Na Eline Maronga
Waombaji
wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu zao
za maombi zimegundulika kuwa na upungufu wameipongeza Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuwapa fursa ya kufanya
marekebisho.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita HESLB ilitangaza orodha ya waombaji wa mikopo kwa
mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu za maombi ziligundulika kuwa na
upungufu na kuwataka waombaji kufika katika ofisi za HESLB jijini Dar es
Salaam na kufanya marekebisho kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka
huu (2015).
Wakiongea
katika ofisi za Bodi leo (Jumatano, Agosti 2, 2015), waombaji hao
wamesema hatua hiyo ya Bodi imewawezesha kurekebisha fomu zao katika
maeneo waliyokosea na hivyo kuweka kumbukumbu zao sawa.
“Mimi
ninaishi Arusha na nilipata taarifa kupitia magazetini na nikatembelea
tovuti ya Bodi na kuona jina langu kuwa sikuweka sahihi… nikaamua kuja
na sasa nimeweka sahihi,” amesema Bw. Sironga Lowassa leo nje ya Ofisi
za HESLB.
Naye
Bi. Enid Mneney, ambaye ni mhitimu wa kidato cha sita katika Shule ya
Sekondari St. Mary Goreth iliyopo Moshi, anasema baada ya kuona jina
lake katika tovuti ya Bodi, aliamua kwenda katika ofisi za Bodi ambako
alifanikiwa kuweka sahihi.
“Mimi
niliona jina langu kwenye tovuti kuwa sikuweka sahihi yangu, nimekuja
na tayari nimeweka sahihi …ninashukuru kwa kupata fursa hii,” amesema
Bi. Mneney mara baada ya kurekebisha taarifa zake katika ofisi za Bodi,
eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi mwishoni mwa wiki iliyopita,
jumla ya fomu za waombaji wa mikopo 7,788 kati ya 68,445 zilizopokelewa
na kuhakikiwa zimegundulika kuwa na upungufu na kuwataka waombaji kusoma
majina yao katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, taarifa muhimu zinazokosekana ni pamoja na
sahihi za waombaji, nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na
picha za wadhamini na baadhi ya fomu za maombi kutosainiwa na
wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama maelekezo yanavyotaka.
No comments:
Post a Comment