Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
Wananchi wa Kijiji cha Moga mara baada ya kuzindua jengo Jipya la Skuli
ya Kijiji hicho la madarasa Manne lililojengwa kwa nguvu za wananachi
wenyewe.
Balozi
Seif akipokea Risala ya Wananchi wa Kijiji cha Moga Mkoa wa Kaskazini
Unguja kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la skuli ya Moja.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza wanafunzi
Nchini kuongeza bidii katika kujifunza masomo yote na kutilia mkazo
zaidi masomo ya Sayansi na Teknolojia ambayo ndio yenye nafasi kubwa
katika harakati za kila siku kwenye karne hii ya Sayansi.
Alisema
katika kuhakikisha juhudi hizo zinafanikiwa, walimu nao wana jukumu
kubwa la kujiendeleza kwa kuwa tayari kujifunza mambo mbali mbali
yanayohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Balozi
Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Wazazi, Walimu na
Wanafunzi wa Kijiji cha Moga baada ya kulifungua jengo jipya la Madarasa
Manne la Skuli ya Msingi Moga iliyopo Wilaya ya Kaskazini “ A ” Mkoa wa
Kaskazini Unguja.
Alisema
Walimu wanahitaji kupatgiwa msaada mkubwa kutoka kwa Wazazi pamoja na
wadau wa Maendeleo katika Sekta hiyo ili skuli zote za hapa Nchini
ziweze kupata mafanikio makubwa zaidi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba juhudi zaidi
zitaendelea kuchukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuzipatia Skuli
vifaa na nyenzo za Kisasa za kufundishia kama vitabu, vifaa vya Maabara,
Komyuta na walimu waliobobea katika fani tofauti ili wanafunzi wawe na
uwezo wa kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.
Alisema
Serikali inatambua kuwa mafanikio ya kweli katika utekelezaji wa
Mipango ya Taifa inategemea jitihada za pamoja kati ya Serikali nyenyewe
na washirika wa maendeleo wakiwemo Wananchi katika kuimarisha Elimu
Nchini.
Alisema
kwamba Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali itaendeleza
kutekeleza dhamira yake ya kuifanya Elimu inayotolewa ianzie katika
ngazi ya maandalizi hadi Sekondari.
Balozi Seif alifahamisha kwamba lengol ni kuihakikisha
kuwa
wanafunzi wote wanaweza kupata elimu ya lazima ya miaka 12 kuanzia
maandalizi hadi Kidato cha Nne sambamba na kuongeza upatikanaji wa
nafasi za kusomea.
Alieleza
kuwa Wazazi na walezi hawana budi kuendeleza kwa pamoja utekelezaji wa
Mipango ya Maendeleo katika kuimarisha Taasisi za Uongozi na uendeshaji
wa sekta ya Elimu pamoja na kuona rasilmali zilizotengwa kwa ajili ya
Sewkta ya Elimu zinatumika kwa ufanisi na kwa kutimiza malengo
yaliyokusudiwa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipongeza juhudi zinazochukuliwa na
Kamati za Skuli Nchini kwa kazi kubwa zinazofanya za kusimamia na
kusaidia shughuli za uendeshaji wa Skuli zao.
Balozi
Seif aliahidi kwamba Serikali itaendelea kuziimarisha Kamati za Maskuli
ili zitekeleze majukumu yake inazojipangia kwa ufanisi mkubwa zaidi kwa
vile Maendeleo yoyote ya elimu yanahitaji msukumo wa pamoja kati ya
Serikali na wadau wake.
Aliiagiza
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuweka mpango wa kuajiri
walimu walio katika maeneo wanayoishi hatua ambayo mbali ya kupunguza
gharama za nauli kwa walimu lakini pia itawapa utulivu wanafunzi kuwa
karibu na walimu wao kwa muda mrefu.
Katika
kuunga mkono juhudi za Wananchi hao wa Kijiji cha Moga Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliahidi kusaidia matofali elfu 2,000
kuchangia ujenzi wa jengo jipya lililoanza kujengwa kwa nguvu za
Wananchi wenyewe.
Balozi
Seif pia akaahidi kusaidia Kompyuta moja na Printa yake kwa lengo la
kuwajengea mazingira bora wanafunzi wa skuli hiyo ya msingi ya Moga
kusoma katika mfumo wa kisasa wa sayansi na teknolojia.
Akitoa
Taarifa za ujenzi wa jengo hilo Diwani wa Wadi ya Gamba Ndugu Machano
Fadhil Babla alisema uamuzi wa Wananchi wa Kijiji cha Moga wa kuongeza
jengo jengine la Skuli umekuja kufuatia matatizo mbali mbali yaliyokuwa
yakiwapata Watoto wao kufuata elimu masafa marefu ya Mkwajuni.
Nd.
Babla alisema watoto wa Kijiji cha Moga walikuwa waki9ata elimu chini
ya Miembe, Madrasa za Quran pamoja na Majengo ya Chama cha Mapinduzi
jambo ambalo lilikuwa haliwapi utulivu watoto hao katika masomo yao.
Diwani
huyo wa Wadi ya Gamba ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kaskazini “A” aliishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar kwa kusaidia ujenzi huo katika hatua za awali licha ya kwamba
Wizara hiyo ndio mkamilishaji wa majengo yote ya skuli yanayoanzishwa na
Wananchi.
Ndugu
Babla alisisitiza kwamba katika kwenda na wakati Kamati ya Skuli,
Walimu na Wazazi wa Kijiji cha Moga wameamua kuendelea na ujenzi wa
jengo jengine Jipya litakalokuwa na madarasa Manne, Maktaba pamoja na
Ofisi ya Mwalim Mkuu.
Akitoa
salamu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Bibi Mwanaid Saleh aliwapongeza Wananchi wa Wadi ya Gamba
kwa uamuzi wao wa kuiunga mkono Wizara ya Elimu katika ujenzi wa Majengo
mbali mbali ya Skul.
Bibi
Mwanaid alisema hatua hiyo ya maendeleo inayofaa kuigwa na Wadi
nyengine hapa Nchini imelenga katika kuwaondoshea changamoto za kupata
elimu watoto wa Taifa hili.
Katibu
Mkuu huyo wa Wizara ya Elimu alilishukuru shirika la Maendeleo la
Sweden { SIDA } kwa juhudi zake za kusaidia gharama za kukamilisha
ujenzi wa jengo hilo licha ya kuendelea kuiunga mkono Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika Sekta ya Elimu hapa Zanzibar.
Ujenzi
wa Jengo jipya la madarasa Manne la Skuli ya Moga lililojengwa kwa
nguvu za Wananchi na kuunga mkono na washirika wa maendeleo wa sekta ya
elimu hadi kukamilika kwake limegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania
Milioni 50,000,000/-
No comments:
Post a Comment