Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika viwanja vya
Kwawazee mjini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwatambulisha na kuwanadi baadhi ya wagombea wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwa majimbo ya Amani na Magomeni katika viwanja vya Kwawazee mjini Zanzibar.

akiwatambulisha na kuwanadi baadhi ya wagombea wa nafasi za Ubunge,
Uwakilishi na Udiwani kwa majimbo ya Amani na Magomeni katika viwanja
vya Kwawazee mjini Zanzibar.
Wafuasi
wa CUF wakimsikiliza mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF Maalim Seif
Sharif Hamad, katika viwanja vya Kwawazee (Picha na Ali Hamad, OMKR)
Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad, amesema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza,
ataifungua Zanzibar kiuchumi na biashara.
Amesema
Zanzibar inazo rasilimali nyingi za kiuchumi lakini bado hazijatumiwa
ipasavyo kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akiwahutubia
wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
viwanja vya Kwawazee kwa ajili ya majimbo ya Amani na Magomeni, Maalim
Seif amesema CUF kina sera imara za kuweza kuleta mabadiliko kwa kipindi
kifupi.
Amesema
tayari ameanza kukutana na baadhi ya makampuni ya uchimbaji wa mafuta,
na kumuahidi kuwa yatashirikiana nae kuhakikisha kuwa azma ya uchimbaji
wa mafuta inatimia muda mfupi baada ya serikali mpya itakayoongozwa na
CUF kuingia madarakani.
Maalim
Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameahidi kuwa
ndani ya siku mia moja za mwanzo za uongozi wake, serikali itakuwa
tayari imeshatunga sera na sheria ya mafuta, ili kuanza rasmi kazi ya
utoaji tenda kwa ajili ya uchimbaji.
Aidha
Maalim Seif amesema atapambana na tatizo la ajira kwa kuwawekea vijana
mazingira ya kuweza kujiajiri na kufanya shughuli zao kwa uhuru bila ya
kuwepo usumbufu wa aina yoyote.
Amesema
iwapo atachaguliwa atatenga na kutengeneza maeneo maalum maalum kwa
ajili ya vijana wa Juakali, na wengine wanaotaka kujiajiri ili waweze
kuendesha shughuli zao za kibiashara na kuongeza kipato chao.
Akizungumzia
mazingira ya uwekezaji, Mgombea huyo wa Urais, amesema ataondosha
vikwazo vyote vinavyowakabili wawekezaji vikiwemo urasimu na rushwa, na
kwamba watapatiwa fursa za uwekezaji muda mfupi kadri itavowezekana.
Ameeleza
kuwa mara nyingi wawekezaji wamekuwa wakipata usumbufu wakati
wanapotaka kuwekeza, na hivyo kupoteza muda mwingi na kukata tamaa,
jambo ambalo serikali atakayoiongoza itasimamia jukumu hilo kuhakikisha
kuwa kila mwenye nia ya kuwekeza anpata fursa hiyo kwa muda muafaka.
Kwa
upande wake meneja kampeni wa Urais wa Zanzibar kupitia CUF, Nassor
Ahmed Mazrui, amesema Maalim Seif ni kiongozi mkweli anayeweza kusimamia
na kutekeleza ahadi zake.
Amesema
iwapo wananchi watamchagua Maalim Seif kuwa Rais wao, milango ya
kiuchumi itafunguliwa Zanzibar na kuifanya kurejea katika hadhi yake ya
kuwa kituo cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Amesema hatua hiyo pia itaongeza ajira na kunyanyua kipato cha wananchi ambacho kitakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi.
Mapema akitoa salamu za wanawake, Bi Nunuu Salim Rashid amewashauri
akinamama
kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kuwashajiisha wengine
kutekeleza haki hiyo kwa wakati, ili lengo lao la kuteta mabadiliko
liweze kufikiwa.
Amesema
bila ya kuichagua CUF katika uchaguzi mkuu ujao, Mamlaka kamili ya
Zanzibar hayatopatikana, sambamba na kurejea kwa katiba inayopendekezwa
ambayo amesema haikuzingatia matakwa ya wananchi.
No comments:
Post a Comment