Maxmillian Rafael Msacky (wapili kushoto) na Patrick James Natala (wa tatu kulia) wakiwa mahakama ya kisutu jana Ijumaa.
Watu
wawili, Patrick Natala na Maxmillian Msacky wamepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 10
yakiwamo ya kughushi, kutengeneza tovuti feki na mifumo ya mtandao kwa
kutumia majina ya Taasisi, viongozi na wanasiasa.
Akiwasomea
hati ya mashtaka jana Wakili wa Serikali, Theophil Mutakyawa
akishirikiana na Wakili Mwandamizi Mkuu wa TCRA, Johannes Kalungura
walidai kuwa washtakiwa hao walitengeneza tovuti feki kwa kutumia majina
ya Taasisi ya Jakaya Kikwete Foundation (Ikulu), TCRA Foundation, Akiba
Saccos Social Company, Social Credit and Loans Company, Ridhiwani
Social Company, Hisa Tanzania, Zitto Kabwe Foundation, Vicoba Tanzania
na Wekeza Fund.
Mutakyawa
alidai kuwa washtakiwa hao wametengeneza tovuti hizo feki kati ya
Januari na Aprili 2014 jijini Dar es Salaam kinyume na kifungu cha 122
(b) cha sheria ya Kielektoliniki na Mawasiliano ya Posta namba 3 ya
2010.
Mbali
na mashtaka hayo, Mshtakiwa Msacky yeye anadaiwa kuwa kati ya 2006 na
2024 kwa njia ya udanganyifu alighushi cheti cha Sekondari namba 0421130
chenye indexi namba S 0260-0001.
Iliendelea
kudaiwa kuwa kati ya 2005 na 2014 mshtakiwa huyo alighushi cheti
kingine cha Sekondari namba 0217951 chenye indexi namba S
0310-0532,akionyesha ni halali na kwamba vimetolewa na Baraza la
Mitihani Tanzania wakati akijua kuwa ni uongo.
Washtakiwa
hao walikana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado
haujakamilika na washtakiwa walipelekwa rumande hadi Septemba 28, 2015
itakapotajwa.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzage alisema kati
ya Aprili na Juni katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 walipata malalamiko
toka kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa makampuni feki yaliyokuwa yakidai
kuwa yanatoa mikopo kwa muda mfupi.
Nzage
alidai kuwa wahusika hao walitumia majina ya wanasiasa na pia kujifanya
ni viongozi na wamiliki wa taasisi hizo na kwamba makumpuni hayo
yanaandaa shughuli za kuchangisha fedha.
No comments:
Post a Comment