Machafuko nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati yamesababisha zaidi ya watu 30 kuuawa mwishoni mwa wiki
Mamia ya
wafungwa katika Gereza moja nchini jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka
wakati ambapo kumekuwa na machafuko yaliyosababisha watu kupoteza
maisha.
Baada ya
Dereva wa Taxi muumini wa dini ya kiislamu kuuawa, mapigano yalizuka
siku ya jumamosi kati ya wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu.
Wafuasi
wa wanamgambo wa kikristo wajulikanao kwa jina anti-balaka walishambulia
gereza siku ya jumatatu, na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi na
wanamgambo.
Jamuhuri
ya Afrika ya kati imekuwa ikikumbwa na machafuko tangu kundi la waasi wa
kiislamu, Seleka kuchukua madaraka mwezi Machi mwaka 2013.
Kundi la Seleka baadae liliondolewa madarakani, hali iliyosababisha machafuko.Maelfu ya watu waliyakimbia makazi yao.
Tangu machafuko mapya kuanza wikiendi, zaidi ya watu 30 wameuawa.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF limesema watoto watatu waliuawa na mmoja kwa kuchinjwa.
Shirika
la habari la AP limesema Watu 500 wametoroka gereza la Ngaragba lililopo
mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui siku ya jumatatu jioni.
Rais wa
mpito wa nchi hiyo Catherine Samba Panza amelazimika kukatiza safari
yake ya kuelekea kwenye Mkutano mkuu wa umoja wa mataifa.
Uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika mwezi Oktoba, mwezi mmoja kabla Baba Mtakatifu Francis kutembelea Bangui.