Uzinduzi wa Kampeni za ADC Gombani Kongwe, Chakechake Pemba - LEKULE

Breaking

11 Sept 2015

Uzinduzi wa Kampeni za ADC Gombani Kongwe, Chakechake Pemba

 MWANACHAMA wa ADC Shamia akisoma Utenzi wakati wa mkotano wa Ufungizi wa Kampenzi za ADC katika kiwanja cha Gombani ya Kale Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 WANACHAMA wa Chama cha ADC Kisiwani Pemba, wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa ADC Mhe:Hamad Rashid Mohamed, wakati alipokuwa akizuna wananchama wa Chama hicho wakati wa ufunguzi wa kampeni katika kiwanja cha Gombani Kongwe kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 MAKAMO mwenyekiti wa Wanawake Taifa Khadija Abdalla Ahmed, akizungumza na wanachama wa ADC katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni wa Chama hicho huko katika kiwanja cha Gombani Kongwe kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 WAGOMBEA wa Ubunge kupitia chama cha ADC kisiwani Pemba, wakiwa wamesima kusubiri kutambulishwa kwa wananchi wakati wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho huko Gombani Kongwe kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 MKURUGENZI wa Habari na Uwenezi wa ADC Taifa Omar Kastan Mtino, akizungumza na wanachama wa ADC wakati wa ufunguzi wa kampenzi za chama hicho, huko katika Uwanja wa Gombani kongwe Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)


 MGOMBEA Ubunge kupitia Chama Cha ADC jimbo la Micheweni Shoka Khamis Juma, akiwaombea kura wabunge wenzake kwa wananchi baada ya kupanda katika jukwaa, wakati wa ufunguzi wa kampeni za Chama hicho huko Gombani Kongwe kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 MAKAMO mwenyekiti wa ADC Zanzibar Faki Khamis Silima, akizungumza na wanachama wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Hicho huko Gombani Kongwe Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA)

 MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC Mhe;Hamad Rashid Mohamed, akizungumza na wanachama wa Chama hicho kisiwani Pwemba, wakati wa ufunguzi wa kampenzi za chama ADC katika viwanja vya gombani kongwe kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA

No comments: