Kumiliki
simu ya mkononi imekuwa si jambo la starehe kama miaka ya nyuma
ilivyokuwa inasadikika. Kadri miaka inavyozidi kwenda kumekuwa na
matoleo mapya ya simu za mkononi na huduma za kipekee zilizo na manufaa
kwa jamii.
Meneja
mkazi wa JovagoTanzania, Bw.Andrea Guzzoni amefafanua kwamba “kadri
matumizi ya simu za kisasa yanavyoongezeka, kunakuwa na huduma tofauti
za malipo kupitia simu za mkononi (Online payments), malipo haya
yameongezeka kwa kasi kubwa kupitia Mpesa, Tigopesa, Airtel money na
malipo ya kibenki (simu banking) ambapo Kenya imeshika nafasi ya kwanza
ikifuatiwa naTanzania katika nafasi ya pili kwa 53% ya huduma hizo za
malipo
Kwa
Upande wake Afisa meneja mawasiliano wa JovagoTanzania, Lilian Kisasa
aliongeza kwa kusema kuwa, pamoja na ongezeko la matumizi ya simu za
kisasa, bado kuna asilimia chache ya watu wanaoweza kutembelea tovuti
mbali mbali kwa lengo la kujifunza na kutafuta huduma za kenye mitandao,
hivyo bado tunahitaji kujiamini katika kutumia huduma za mitandaoni
kwani kuna baadhi ya tovuti hazina utapeli na zina faida kwa jamii.
Hata
hivyo, soko hili la simu linabadirika kila baada ya mwezi, mwaka au
miaka miwili, kwa kipindi cha nyuma kulikuwa na matolea ya zamani ambazo
simu nyingi zilikuwa na uwezo mdogo wa internet na kumfanya Mtanzania
kupata wakati mgumu iwapo atahitaji huduma yeyote ya mtandaoni. Lakini
kwa hivi sasa kumekuwa na tano bora ya simu za kisasa ambazo
zinanunuliwa kwa kasi ambazo ni Samsung, Nokia, na Iphone, simu hivi ni
chachu ya maendeleo katika jamii, “bado tuanaamini hivyo kwa kuwa
zinauwezo mkubwa wa kutoa huduma yoyote kupitia playstore au ios
kutegemea na hitaji la mtumiaji” alifafanua.
Hata
hivyo, kutokana na takwimu zilizofanywa na jovagoTanzania, Kampuni
inayojihusiha na soko la mtandaoni, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko
la 15% katika nchi za Afrika ya mashariki na kukadiriwa kutakuwa na
ongezeko la zaidi ya 33% katika miaka mitatu ijayo. Kwa sababu hiyo,
bado kuna nafasi kubwa ya watanzania kunufaika na ulimwengu huu wa
kidigitali kwa kupata huduma tofauti za mitandaoni zitakazoendelea
kujitokeza kila mwaka , mfano kwa sasa mtanzania anauwezo wa kuagiza
chakula kupitia Hellofood, kununua mavazi au bidhaa za ndani kupitia
Kaymu na kubook vyumba vya hotelini kutoka Jovago.com kwa simu zao
mkononi.
No comments:
Post a Comment