TANESCO MNAUONA HUU MTO - LEKULE

Breaking

19 Sept 2015

TANESCO MNAUONA HUU MTO


Nyuma yangu ni sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuzalisha umeme ila bado hauna manufaa kwa wakazi wengi kwani ni mdogo mno.Nilifika eneo hili miaka ya nyuma kidogo katika shughuli zangu za kulijenga Taifa langu pendwa Tanzania.

Tanesco nimeamua kuwaonyesha huu mto ni mto Ruvuma mkoani Ruvuma ebu tatueni tatizo la umeme katika mkoa huo tajwa ila wakazi wa Songea Ruvuma na mikoa jirani nao wafurahie uwepo wa mto huu na kupata hamasa ya kuutunza.Ni wangu mtazamo tu Tanesco kwa wangoni hawa wa Kitanzania.

Kuna mradi upo pale unaendelea kwa sasa wa umeme lakini nahisi bado hauna manufaa kwa wanalizombe wa Songea, kwa kuwa ni mradi wa taasisi binafsi ya Watawa wa kanisa Katoliki,nendeni mtie mikono yenu pale muongeze ufanisi na utendaji kazi wake uwanufaishe watu wengi zaidi.

No comments: