Taarifa Ya CHADEMA-US Kukanusha Mbowe Kujisalimisha Kwa Dr. Slaa - LEKULE

Breaking

19 Sept 2015

Taarifa Ya CHADEMA-US Kukanusha Mbowe Kujisalimisha Kwa Dr. Slaa


Napenda kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa ya uongo na uzushi iliyoenezwa kupitia mitandao ya kijamii  tarehe 18 Septemba 2015 iliyoanzia kwenye JamiiForums yenye kichwa cha habari “Mbowe asalimu amri kwa Dr Slaa”. 
 
Katika taarifa hiyo mwandishi amenitaja mimi Kalley Pandukizi kama mmoja wa viongozi wa CHADEMA tawi la DMV pamoja na viongozi wenzangu kuwa tumewapokea viongozi hao wa juu hapa Marekani na wapo katika hoteli moja Ohio kwa ajili ya mazungumzo binafsi.

Napenda kueleza umma kuwa taarifa hii si ya kweli, ni ya uongo na uzushi yenye lengo la kuhadaa umma wa Watanzania kuwa kuna mazungumzo kati ya viongozi hawa hapa Marekani. 
 
Pia ina lengo la kunichafulia jina mimi kama Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la DMV.

Mwisho napenda kutoa wito kwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA pamoja na UKAWA kwa ujumla wake, kupuuzia taarifa kama hizi zenye lengo la kupotosha na kuhadaa umma kwa malengo mabaya ya kisiasa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

Imetolewa na:-

Mwenyekiti wa CHADEMA - DMV, Marekani

Kalley Ammy Pandukizi

No comments: